Aina Tatu Za Watu: MOTO, BARIDI NA UVUGUVUGU


Leo ni terehe 09 Julai 2018. Hongera sana rafiki ya kwa siku hii ya kipekee sana. Haijawahi kutokea  haitakuja kutokea.

Moja kati ya usemi ambao ni rahisi sana kuusikia kutoka kwa vijana ni usemi kama huu hapa.

 YAANI SIKU HIZI KWENYE KUANGALIA MOVIE SIPO,….KWENYE KUANGALIA MPIRA SIPO…..YAANI NIPO NIPO TU.

Bila shaka umewahi kusikia usemi huu mara nyingi sana, sana. Na pengine inawezekana wewe mwenyewe unasema hivi.

Soma Zaidi Hapa: Nani Ametengeneza Kanuni Hii? Haifanyi kazi!!

Yaani kiufupi kwamba wewe sio wa moto, wala sio wa baridi. Upo upo tu!

Kiukweli kauli hii japo inatamkika kirahisi lakini inashangaza sana. Maana hii ni dalili ya mtu ambaye hajielewi wala haelewi wapi anatoka na wapi anaelekea.

Hii ni dalili ya kuishi, ishi sio dalili ya kuishi.

Rafiki yangu kabla hujaendelea kusoma hapa naomba ujiulize swali, hivi kama sasa hivi utaulizwa kitu kimoja ambacho unafanya utasema nini?

Je, kama utaulizwa kitu kimoja ambacho huwezi kupitisha siku bila kufanya ni kipi?

Au upo upo tu. Huu uvuguvugu wa kuwepo kuwepo ni mbaya sana. Na ili kuondokana nao, basi hakuna jinsi isipokuwa ni kuwa MOTO AU BARIDI.

Kuwa moto ni kuwa na hamasa ya kufanya kitu, na kuhakikisha unakifanya bila kujiuzuia. Msukumo wa wewe kufikia malengo yako unakuwa mkubwa sana unapokuwa moto.

Ukiwa moto kikitokea kikwazo cha kukuangusha kinakuwa kama kimekupiga teke na kukusogeza mbele zaidi. Ukiwa moto kiufupi unakuwa hauzimiki.

Ukiwa BARIDI unasinyaa muda wote. Huchukui hatua, badala yake unasubiri watu wachukue  hatua ili uwakosoe. Furaha yako inakuwa kuona watu wanachukua hatua na kushindwa.

Na katika maisha tuna chaguo moja tu kati ta hayo. Kuwa MOTO au kuwa BARIDI. Lakini sio uvugu vugu.

Kati ya machaguo hayo kuwa MOTO ndio chaguo bora zaidi.

Lakini uvuguvugu ni ishara ya kutokueleweka wapi unaenda. Ndio hapo unapotokea usemi wa mimi nipo nipo tu.  Hawa ni watu wa uvugu vugu. Hawana uhakika kama wasonga mbele au wanarudi nyuma. Hawana uhakika kama wanakimbia au wanatembea. Hawana uhakika kama wanapenda au wanachukia. Hawana uhakika kama wanafuraha au wamehuzunika.

Kwa maelezo haya hapa, kama tungekuwa tunagawa watu katika aina basi tunazo aina tatu.

Kuna watu ambao ni moto
Wengine ni baridi.
Na aina ya mwisho ni watu uvuguvugu.

Kati ya hizo kuwa moto ni bora sana, sana. Na kuwa uvuguvugu ni hatari zaidi.

Asante sana rafiki yangu. Chagua kuwa moto na kuwa MOTO kweli.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X