Athari Ya Mtazamo Wako Kwa Vitu Vinavyokutokea


Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii njema ya leo. Ianze siku ya leo ukiwa na mtazamo chanya wa kushinda. Mtazamo wa kufanya makubwa na mtazamo wa kukutana na mambo mazuri.

Kwa nini kuwa na mtazamo kama huu? Hili ni swali ambalo kwa haraka haraka unapaswa kuliuza.

Kiukweli ni kwamba mtazamo chanya ndio utaleta mwitikio wako kwa kile unachokutana nacho.

Kama kama mtazamo wako leo ni kwamva LEO NI SIKU NJEMA SANA. Kiukweli hata ukikutana na kitu kibaya kikautokea (na uwezekano wa kutokea upo) hautayumbishwa.
Mtazamo wako chanya hauwezi kuharibiwa na hali ya hewa, kwamba ni baridi, joto, mvua au jua kali.
Kama utaamka na mtazamo chanya haijalishi humu katikati kutatokea nini bado utaendelea tu kujiona wewe ni mshindi.

Soma zaidi: Uchambuzi Wa Kitabu:  FAILING FOWARD; Ukianguka Angukia Mbele

Mtazamo chanya  unaweza kukufanya uzione fursa au usizione kabisa.
Mtazamo chanya utakufanya upate ushindi hata pale maisha yanapokupuga teke. Kwa kawaida tunategemea maisha yakikupiga wewe uanguke. lakini mtazamo chanya unaweza kukufanya upigwe teke na kusogea mbele badala ya kurudi nyuma.

Mtazamo chanya unaweza kukufanya ukipigwa teke uanguke chini, lakini tofauti na kuanguka kwa watu wa kawaida. Wewe unaanguka chini unaokota kitu na kuendelea kutembea nacho.

Rafiki yangu badala ya kuanza kulalamika maisha ni magumu, au kuona serikali inabana. Wewe anza kuviangalia vitu hivi kwa jicho la tofauti. Jicho la UCHANYA. Binafsi jicho hili huwa napenda kuliita jicho la dhahabu. Yaani jicho linalokufanya uone uzuri wakati wengine wote wanalia.

Ukitaka kujua umuhimu wa mtazamo chanya,
Muulize kocha wa mpira wa miguu dakika chache kabla ya mechi, jinsi mtazamo chanya wa timu ulivyo na madhara kwenye ushindi

Au muulize daktari ni kwa jinsi gani mtazamo chanya wa mgonjwa unavyoweza kumponya au kumuua mgonjwa

Au muulize mwalimu jinsi mtazamo chanya wa mwanafunzi unavyoweza kusababisha ushindi au kushindwa kwa wanafunzi wake.

Kiujumla naomba nimalizie kwa kusema hivi.
Kama unafikiria vitu vizuri, basi vitu vizuri vinakufuata.
Lakini pia kama mtazamo wako ni kupata mabaya, basi na yenyewe hayana huruma. Yatakufuata tu.
Ipo hivyo na inafanya kazi. Kama huamini jaribu kujipa siku 30 tu ambapo wewe utategemea mambo mazuri sana kutoka kwenye kile unachofanya. Siku 30 za kuwa na mtazamo chanya. Utashangaa sana, matokeo utakayopata.

Soma Zaidi: Hawa Watu Walipaswa Kuwa Wamefukuzwa Kazi

NB. Mtazamo chanya unapaswa kuendana na kuchapa kazi. Sio tu unakaa na kusema nina mtazamo chanya huku hufanyi kitu chochote.

Ni hayo tu rafiki, kwa leo nakutakia siku njema sana.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X