Hii Ndio Sifa Ambayo Kila Kiongozi Anabeba


Mara nyingi sana likiongelewa neno kiongozi basi kinachokuja kwenye akili za watu walio wengi sana ni mtu mwenye mamlaka au madaraka.

Kwa maana ya kawaida ambayo inatumiwa na watu wengi sana. Basi kiongozi ni mtu ambaye ana cheo katika shirika, kampuni au taasisi fulani. Lakini je hii ni kweli?

Vipi nikisema hata mfagia barabara ni kiongozi. Au nikisema katibu kwenye ofisi fulani naye ni kiongozi? Je, utanielewa kweli hapa?

Sasa hapa naomba nitoe maana fupi ya kiongozi. Kiongozi ni mtu yeyote aliye hai. Binafsi napenda maana ya kiongozi ikae hivi.

Soma zaidi: uchambuzi wa kitabu: THE ALCHEMIST

Mtu yeyote anayeishi duniani. Ni kiongozi. Uongozi unaanza pale unapozaliwa siku ya kwanza na kadri unavyokua majukumu yako ndivyo yanazidi kuongezeka.
Mfano mtoto mdogo anavalishwa nguo, lakini akikua yeye kama kiongozi basi anapaswa kuhakikisha kwamba anajivisha nguo. Hapo majukumu yanakuwa yameongezeka zaidi ya awali. Kwa hiyo kiufupi ni kwamba kadri kila mtu anavyozidi kujitambua ndivyo majukumu yake kama kiongozi yanazidi kuongezeka zaidi.

Sasa naomba nisirefushe sana mada, kwa leo kikubwa napenda ujue sifa kubwa ambayo kila kiongozi anayo. Na sifa hii sio nyingine bali ni kujifunza.  Kiongozi mzuri ni yule ambaye anakaa chini na kujifunza kwa kusoma vitabu juu ya mambo ambayo wanafanya viongozi wengine. Anajua viongozi wengine wamewezaje kufanikisha vitu fulani kwenye maisha na jinsi yeye mwenyewe anaweza kuvifanikisha. Hii ndio sifa muhimu ya kiongozi.

Je, wewe unafanya hivi? Kama ulikuwa bado hujifunzi kwa kusoma vitabu basi leo hii badilika. Anza kujifunza. Anza kusoma na anza kutafuta maarifa mapya yatakayokuwezeha kufanya kazi kwenye viwango vya hali ya juu sana.

Soma Zaidi: Kijana Usidanganyike, Wakati Unazidi Kusogea

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X