Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii njema sana ya leo.
Ni mara nyingi sana umekuwa ukiambiwa na watu juu ya biashara ambazo unapaswa kufanya. Ni mara nyingi sana umekuwa ukizisikia fursa muhimu sana ambazo unapaswa kuzikimbilia zikakuinua kutoka hapo ulipo kwenda hatua ya ziada.
Lakini ni mara chache sana umekuwa ukisikia juu ya biashara ambazo hupaswi kufanya haswa kutoka kwangu. Hii inatokana na sababu kwamba mara nyingi huwa siongelei vitu hasi, hivyo kila wakati kusisitiza juu ya mambo chanya.
Soma Zaidi; Haya Ni Malalamishi Unayopaswa Kuwa Nayo
Hata hivyo, leo nimelazamika kukwambia juu ya biashara ambayo hupaswi kuifanya ili mwisho wa siku usije ukajiingiza kwenye biashara hii. Maana sio biashara nzuri na haitakusogeza mbele kwenye maisha yako.
Biashara hii sio nyingine bali ni biashara ya KUKATISHA WATU TAMAA.
Hii ni biashara ambayo hupaswi kujihusisha nayo kabisa. Acha watu wengine wahangaike na bishara hii ila sio wewe. Ukiona mtu anakuja kwako na kukushirikisha ndoto yake, mheshimu sana sana.
Usimkatishe tamaa hata kama utakuwa unaona HAIWEZEKANI. mpe nguvu, mtie moyo na kila wakati mkumbushe juu ya kupiga hatua za kuielekea ndoto yake.
Wewe unaweza kuwa unaona kwamba haiwezekani lakini mwisho wa siku yule akawa ameifikia. Na siku zote mambo yamekuwa yanaenda hivi. Kile ambacho wewe huwa unaona hakiwezekani, mwisho wa siku ndio huwa kinakuja kuwezekana.
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba “hakuna kitu kinaumiza kama pale unaposema kwamba haiwezekani, wakati huo huo ukapitwa na mtu mbele yako anafanya kile ulichosema hakiwezekani”. Kwa hakika mtu huyu alikuwa sahihi.
Hakuna kitu kitakuja kukuonesha kwamba hukuwa sahihi, kama siku ile utakapopitwa na mtu anayefanya kitu ambacho wewe siku zote umekuwa unaamini hakiwezekani.
Ni hayo tu rafiki yangu, nakutakia siku njema sana.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391