Hii Ni Kauli Ambayo Unapaswa Kuiepuka Kwenye Maisha Yako


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana, sana kwa siku hii ya leo.

Tangu tunapoamka asubuhi mpaka jioni huwa tuko kwenye maongezi. Na maongezi huwa tunayatumia kama njia ya kuwasiliana na watu wengine. 

Maongezi haya huwa yanakuja kupitia kauli tunazotoa.

Na mara nyingi sana watu huongea na kutoa kauli bila kufikiri. Kitu ambacho baadae huwa wanakuja kujutia.

Hata hivyo leo napenda uijue kauli moja tu ambayo utapaswa kuiepuka kwenye maisha yako. Na kauli hii sio nyingine bali kauli ya BORA YA JANA.

Hivi ni mara ngapi huwa unatoa kauli hii hapa maishani mwako. Au ni mara ngapi wewe unasema KILA KUKICHA BORA YA JANA.

Rafiki, sichelewi kukwambia kwamba hii ni kauli ya wazembe.

Soma zaidi:  KONA YA SONGA MBELE; Hii Ni Kauli Inayodidimiza Ubunifu Barani Afrika

Maana kila siku ni siku bora sana kuliko jana. Hivyo jana haiwezi kuwa bora zaidi ya leo hata siku moja.

Tunapoamka asubuhi tunakuwa wapya, tunakuwa kama tumezaliwa na mbinu mpya, mawazo mapya nk.

Hivyo vitu hivi tunapaswa kuhakikisha tunavitumia vyema kabisa ili kuifanya leo kuwa bora zaidi ya jana.

Kuanzia leo achana na kauli ya BORA YA JANA. Hakikisha unaiishi leo katika ubora wake kwa kufanya kile ambacho unapaswa kukifanya.

Ni hayo tu rafiki kwa siku ya leo. Asante sana, tukutane kwenye meza tetu ileee ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X