Hii Ni Nafasi Ambayo Unapaswa Kuishikilia Siku Zote


Niliingia katika mfumo wa elimu kama mwanafunzi miaka takribani 16 iliyopita. Kwa mara ya kwanza nikiwa shule ya msingi baada ya kufanya mtihani wa kwanza matokeo yalitolewa. Walianza kusoma matokeo. Kwangu hili lilikuwa jambo geni ambalo nilikuwa sijawahi kukutana nalo maishani.

Katika matokeo hayo kulikuwa na nafasi ya kwanza mpaka ya mwisho.
Kwa jicho la haraka niligundua matokeo yalikuwa yamegwanyika katika sehemu kuu tatu.

Sehemu ya kwanza ni wanafunzi watatu wa kwanza.  Hawa walipigiwa makofi na kupewa zawadi za daftari na kalamu.

Sehemu ya pili ni wanafunzi kumi waliofuata. Hawa walipigiwa makofi tu.

Sehemu ya tatu ni wanafunzi waliobaki. Hawa hawakupigiwa hata makofi.

Sasa wakati nafuatilia mambo hayo yote ndipo nilikuja kugundua kwamba MTU WA KWANZA NDIYE ALIYEPEWA THAMANI ZAIDI.

Jambo kama hili linajitokeza kila siku kwenye maisha. Wa kwanza ndiye anapewa thamani kubwa sana.

Angalia makampuni ya simu. Kampuni linalotoa simu zenye ubora, watu wapo tayari kuhakikisha kwamba wananunua simu zake, hata kama ni gharama sana.

Mtu mwingine anataka kununua simu ya kampuni fulani tu kwa sababu kampuni hiyo ndio inayotoa thamani ya hali ya juu sana. Rafiki yangu, naomba nikwambie kitu. Katika maisha mtu wa kwanza ndiye anayepewa kipaumbele sana kuliko mtu mwingine.

Siku zote pigana kuhakikisha unakuwa wa kwanza katika kile unachofanya.

Kwa nini kuwa kwanza?
Kwanza ukiwa wa kwanza ni kipimo cha thamani kubwa sana ambayo umeitoa.

Pia kuwa wa kwanza ni ishara kwamba unautumia vyema uwezo wako ulio nao kwa viwango vikubwa sana.

Na mwisho kuwa ukiwa wa kwanza utakuwa umegusa maisha ya watu walio wengi sana, sana.

Sasa, kuna kitu kimoja pia napenda ukifahamu. Kitu hiki ni kwamba KAMA WEWE SIO WA KWANZA BASI WEWE NI WA MWISHO. Hilo tu baasi.
Kwa hiyo jitahidi kuwa kwanza maana bila hilo ndio kusema kwamba wewe utakuwa wa mwisho.

Asante sana rafiki yangu.
Endelea kusoma makala za kuhamasisha na kuelimisha kutoka kwenye blogu hii hapa.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X