Hiki Ni Kitu Ambacho Huwafanya Watu Wengi Kushindwa


Habari ya siku hii njema sana rafiki na ndugu msomji wa blogu yako ya songa mbele. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako na unaenda kufanya mambo makubwa sana ndani ya siku hii ya leo.
Leo hii tunaenda kutafakari kitu ambacho watu huwafanya watu wengi kushidwa, kuanguka na kuacha kufikia ndoto zao.
Watu wengi sana wakiwa wanaanza kitu huwa wanaanza kwa nguvu kubwa sana. Yaani huwa wanakuwa na moto mkubwa sana kiasi kwamba huwa inakuwa ni vigumu kuwazuia. Kama ni biashara basi unakuta mtu anakwambia yaani hii fursa ndio yenyewe, mimi nakomaa nayo mpaka kieleweke. Kama ni mahusiano basi unakuta watu hawazuiliki kila wakati wanapenda kuwa wote na kufanya vitu kwa pamooja.

Yaani kama ungekuwa ni moto unaweza kusema kwamba basi huo moto unakuwa umechochewa kwa kuni kavu ambazo zinawaka kwa kasi kweli.
Lakini kama ilivyo kawaida, uzuri wa kitu au ubaya wa kitu huwa hauonekani kwa kukiangalia tu, bali pia kwa kutumia kitu hicho. Ndio maana wahenga huwa wanasema kwamba utamu wa ngoma sharti uingie ucheze. Sasa baada ya watu kuingia kwenye ulingo ndipo huwa wanakutana na vikwazo pamoja na vuta na nikuvute. Hapo ndipo kazi huanza. Hapa ni wachache sana huwa wanaweza kuhimili hapa na kuweza kuendelea mpaka mwisho.
Kwa nini?
Ili kitu chochote kiwepo, kunahitajika gharama ya kulipa. Kwa mfano ili uweze kutembea na hatimaye kufika kwenye kilele cha mlima basi utahitaji kulipa gharama. Na hapa ninapozungumzia gharama rafiki yangu naomba tu unielewe vizuri. Hapa simaanishi pesa tu. Ndio pesa inaweza kuwa sehemu ya gharama lakini sio gharama peke yake. Gharama hii inahusisha kujitoa, kufanya kazi kwa bidii, kutokuangalia nyuma na kuendelea kuchochea moto mpaka pale moto unapokuwa umekuwa moto kweli. Rafiki yangu, kama unataka kwenda kufika unapotaka kufika lazima uwe tayari kulipa gharama.
Sasa watu wengi ambao huwa wanashindwa ni kwa sababu huwa wanashindwa kulipa gharama ya kitu husika. Ndio maana wengi huwa wanaanza vitu na kuishia njiani. Mtu anayeanza kupanda mlima na kuishia njiani, haiishii tu njiani kwa sababu ya kitu kinginie bali kwa sababu ya kusihidnwa kulipa gharm
Mtu anayenzisha biashara kuiacha baada ya siku chache sana, haishii tu njiani kwa sababu ya kitu kingine bali kwa sababu ya kushindwa kulipa gjarama. Hivyo kwa mtu ambaye hayuko tayari kulipa gharama basi ni vigumu sana kuweza kufanikiwa na kufika kule ambako anataka kufika,
Johna Mason aliwahi kuandika kwamba watu wengi sana wanaoshindwa kwenye maisha, huwa hawashindwi kwa sababu kuna mtu anawavuta, bali kwa sababu  wamepata ushindi kidogo na kudhani wamefika mwisho. Je, rafiki yangu unafikiri hii inatokana na kitu gani. Hii inatokana na ukweli kwamba watu walio wengi wanakuwa tayari kulipa gharama mara ya kwanza lakini wanashindwa kuendelea kulipa gharama.

Iko hivi rafiki, kadri unavyokuwa unalipa gharama, ndivyo unapaswa kulipa gharama zaidi na zaidi. Na kadri unavyopanda ndivyo unapaswa kulipa gharama nyingine zaidi na zaidi. Hakuna kitu kwamba unavyopanda unapunguza kulipa gharama. Hapana huo ni uongo na ni kukwepa wajibu wako wewe kama wewe.
Chukulia mfano mdogo wa kwenye familia. Mtoto anapokuwa mdogo anakuwa anapewa kila kitu. Chakula analishwa, kinywaji anapewa. Nguo anavalishwa n,k
Inafikia hatua wazazi wanapika chakula na kuandaa kinywaji na mtoto anapaswa kujilisha, kunywa mwenyewe na kuvaa nguo yeye mwenyewe bila msaada wa mzazi, hapa anaanza kulipa gharama. Kadri siku zinavyokuwa zinasonga mbele inafikia hatua ambapo sasa yeye anapaswa kutafuta chakula, inabidi atafute mavazi ya kwake na pengine mtoto huyo anapata familia na kupaswa kuigharamikia zaidi na zaidi.
Kumbe gharama sharti ilipwe.  Na hapa hatuoni sehemu ambapo ukuaji wa mtoto unaambatana na kupungua kwenye kulipa gharama, bali ukuaji wa mtoto unaendana na gharama ambayo anapaswa kuhakikisha kwamba ameilipa. Hivyo rafiki yangu. Kama kuna kitu kimoja ambacho ninapaswa kukwambia ndani ya siku hii ya leo, basi ni utayari wako katika kulipa gharama. Kiufupi ni kwamba unapaswa kuwa tayari kulipa gharama, lipa gharama na lipa gharama. Yaani hakuna jinsi unavyoweza kufanikiwa na kufikia kwenye kilele cha mafanikio bila ya wewe kuwa tayari kulipa gharama.
Sasa katika makala haya ya siku hii ya leo naomba tuondoke na vitu hivi hapa vinne.

1.      Ili ufanikiwe na uweze kufikia kwenye kilele cha mafanikio basi unapaswa kulipa gharama

2.       Gharama inapaswa kulipwa kila wakati

3.       Kadri unavyopanda ngazi, ndivyo unapaswa kulipa gharama zaidi.

4.       Kupanda, kubadilika na kushuka pamoja na kulalamika vinahitaji gharama vyote, ni juu yako kuamua ni wapi ulipe gharama zaidi. Unaweza kuamua kulipa gharama ya ushindi, au ukaamua kulilpa gharama ya kushindwa. Uamuzi ni wako, ila gharama ni ile ile.  Maana kamam tulivyoona hapo juu, ukitaka kushinda lazima ulipe gharama, na kama kushinda zaidi unapaswa kulipa gharama zaidi. Vivyo hivyo kwa kushiindwa, kama unataka kushindwa, unapaswa kulipa gharama, kama unataka kuhsindwa zaidi utalipa gaharama zaidi ya kushindwa. Ila gharama ipo tu hakuna siku siku utaikwepa uwe unataka kushinda au kushiindwa.

Asante sana rafiki yangu mpendwa. Imani yangu suala zima la kulipa gharama utaanza kuliafnyia kazi na kuhakikish kwamba unalipa gharam inayotakiwa ili uweze kufika kwenye kilele cha mafaniko ambayo unataka. Asante sana, tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


One response to “Hiki Ni Kitu Ambacho Huwafanya Watu Wengi Kushindwa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X