Habari ya siku hii njema sana rafiki. Hongera kwa uhai wa siku hii nyingine. Kama ishara ya kujipongeza naomba uvute pumzi kwa nguvu mara tano.
Sasa tuendelee. Kila siku unakutana na watu wapya. Na pengine unakutana na watu walewale ambao umewazoea. Je, umeshajiuliza ni kitu gani unapaswa kukitafuta kila unapokutana na mtu. Je, ni kitu gani hiki unapaswa kukiangalia?
Unapaswa kuangalia upande wao wa ushindi. Je, wamewezaje kushinda? Je, wamefanyaje kupata kitu fulani. Kila mtu kuna kitu fulani ambacho ni kidogo sana ambacho anakiwezea sana. Sasa kitu hicho ndicho unapaswa kukitafuta jinsi walivyokiwezea na kupiga hatua kubwa sana.
Jifunze kwa kila mtu, tafuta kitu chanya na endelea kusonga mbele.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391