Hivi Ndivyo Watu Wanaweza Kufikia Malengo Makubwa Sana


Je, una lengo kubwa sana kiasi kwamba unajiuliza nitalifikiaje? Je, umepabga kulifikia baada ya muda gani?

Hongera sana kwa kuwa lengo kubwa kama hili hapa. Ila sasa tunapaswa kuzungumzia juu ya saikolojia ya kuhakikisha wewe unalifikia lengo lako.

 Sasa ni muda wa kuingia kwa ndani na kuangalia mambo ambayo watu hufanya katika kuhakikisha kwamba wanafikia malengo yao.

Soma Zaidi: 365 Anza Kutumia Kile Ulichonacho
Kama kuna mtu ambaye umewahi kumwona amefikia malengo yake makubwa sana, usishangae alifanyaje, ni rahisi sana na wewe unapaswa kufanya hivi. Ni kwamba siku zote huwa anafanya kitu kidogo kuhakikisha anafikia lengo lake.  Kwa hiyo kwake kila iitwayo leo anafanya kitu kuhakikisha anafikia lengo lake. Hivi ndivyo watu wote waliofikia ndoto na malengo yao walivyofanya.

Yaani hatua moja kila kukicha. Sasa na wewe anza kufanya hivi. Cha kufanya andika lengo lako chini haraka iwezekanavyo. Baada ya hapo jipe kazi ya kufanya vitu vidogovidogo sita kila siku kuelekea lengo. Kila kukicha wewe fanya vitu vidogo sita kwa mwaka mzima. Nina hakika baada ya mwaka hutakuwa mahali hapo tena. Yaani utakuwa umepiga hatua kubwa sana kuliko kawaida.

Rafiki yangu kazi ya kufanya siku ya leo. Andika malengo yako chini.
Chagua lengo moja ambalo unaona kwamba hili ndilo lenyewe la kuanza nalo.

Jiulize mambo madogo sita utakayiyafanya ndani ya siku hii ya leo amabayo yatakusogeza kwenye kilele cha lengo lako.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X