Habari ya siku hii njema sana ya leo rafiki. Hongera sana kwa siku hii njema ya leo rafiki yangu. Hakika leo ni siku ya kipekee sana, basi hakikisha unaitumia vyema ili uzidi kusonga mbele.
Moja kati ya watu wanaofikia mafanikio makubwa sana kwenye dunia hii ni watu WABISHI. Wabishi ni watu ambao wanafurahia sana mema ya dunia hii.
Naomba tuelewane tangu mwanzo kwamba neno ubishi linavyotumika siku ya leo halimaanishi kurushiana maneno kutaka kujua nani anaujua mpira zaidi ya mwenzake. Pia neno ubishi halimaanishi kukataa mawazo ya watu wengine, au kukataa kushauriwa na watu.
Ubishi unaozungumziwa ni ile hali ya kutotulia mpaka pale unapokuwa umepata kile unachokihitaji. Ubishi wa kutokukubali kushindwa hata kama dunia inakukatalia na inakupa sababu lukuki za kwa nini wewe umeshindwa tayari.
Soma Zaidi: Vitu Vitatu Vitakavyoongeza Ufanisi Kazini Kwako
Rafiki yangu, dunia siku zote itakupa sababu zote hizi, za kwa nini wewe umeshindwa na huwezi kusonga mbele. Lakini habari njema ni kwamba kama utaendelea kuonesha ubishi wako lazima tu utaweza kufika unapotaka kufika.
Moja kati ya ubishi muhimu sana ambao unauhitaji ni ubishi wa kutokukubali matokeo madogo. Na ili ubishi huu ulete maana, basi unapaswa kuweka juhudi kila wakati kuhakikisha unapata matokeo makubwa sana. usikubali kupata matokeo madogo wakati una uwezo wa kupata kitu kikubwa sana zaidi ya hicho ambacho unacho sasa hivi.
kuwa mbishi. Dunia ikikwambia inatosha. Wewe onesha kwamba bado sana haijatosha.
Dunia ikikwambia huwezi kufika kule wewe ongeza kasi ya kukimbia ili ufike.
Dunia ikisema fulani alishindwa, basi ubishi wako uwe wa kuonesha kwamba wewe utakuwa mtu wa kwanza kufanya makubwa zaidi ya hapo.
Huu ni ubishi muhimu sana ambao unapaswa kuuonesha.
Na ubishi ambao unapaswa kuukataa maisha yako yote ni ubishi wa matokeo madogo. Wewe sio mdogo na usikubali matokeo madogo.
Asante sana rafiki yangu. Nikutakie wakati mwema sana rafiki. Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391