Jambo Moja Ambalo Halipaswi Kukushangaza


Mara nyingi sana huwa tunaamua kufanya vitu na watu mbali mbali. Huwa tunanda makundi ili kufanya kazi pamoja na watu n.k,

Na mara nyingi sana huwa tunaweka nguvu yetu kubwa sana huko tukifahamu kwamba makundi haya tuliyoyaunda yatadumu milele. Na mara makundi yanapoleta dosari au kuonesha hali ya kutoeendelea basi watu hukata tamaa na kuona kwamba wamesalitiwa.

Ukweli ni kwamba wasaliti watakuwepo katika kila eneo ambalo utakwenda.

Kwa hiyo jambo hili halipaswi kukushangaza. Yaani usiweke nguvu na akili yako kwa kuwaamini watu unaokaa nao au unaofanya nao kazi kwa  asilimia 100.

Waamini kwa kiwango fulani na kiwango fulani ujue kabisa kwamba muda wowote wanaweza kukusaliti. Hivyo rafiki yangu ukilifahamu hili hapa, hautapata taabu hata kidogo pale litakapotokea baya kwenye mahusiano au kikundi chako.

Ukweli ni kwamba uwezekano wa watu kukusaliti, au kukuacha upo tena mkubwa tu. Ila hili halipaswi kuwa jambo la kukushangaza.

Asante sana rafiki yangu,  kafanyie kazi hili hapa.

Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.


One response to “Jambo Moja Ambalo Halipaswi Kukushangaza”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X