Jambo Moja Unalopaswa Kufahamu Kabla Ya Kuingia Kwenye Mahusiano


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo.
Rafiki yangu naomba niikwambie kwamba tupo katika dunia hii kuhakikisha kwamba tunafanya mabadiliko makubwa sana. hii ndio kusema kwamba hatupaswi kuwa watu wa kufanya kitu ilimradi tu tumefanya au kuonekana kwamba tumo. Bali tunapaswa kuhakikisha kwamba tumekifanya kwa kuweka nguvu na moyo wetu pale.  Hivyo leo hakikisha unaishi kanuni hii na unafanya mabadiliko kwa kitu hata kama ni kidogo. Ukiona umeenda kulala bila kufanya kitu chenye maana kubwa sana, basi ujue wewe upo hapa duniani ili kula na kunywa tu. Jambo ambalo hata kuku na ng’ombe wanafanya kila siku. Ebu jitahidi kuwa wa tofauti.
Sasa turudi kweenye  makala ya leo
Tunapozungumzia suala zima la mahusiano, basi ni jammbo ambalo haliepukiki. Tunaishi katika dunia ambapo kuhusiana ni lazima. Iwe ni uhusiano na rafiki zako, jamii, familia n.k
Kiukweli tunaishi katika ulimwengu ambapo hakuna mtu ambaye hana uhusiano. Na uhusiano huu unaweza kuwa ule ambao wewe kama unajikuta tu na hauwezi kuubadili lakini pia unaweza kuwa ule wa wewe kuanzisha.
Kwa mfano uhusiano wako wewe na wazazi wako wako ni uhusiano ambao wewe kama wewe hauna kitu chochote cha kubadili. Umejikuta kwamba wewe umezaliwa na baba na mama fulani basi. Hapa hakuna kubwa sana ambalo unaweza kubadili isipokuwa ni juu yako kuhakikisha kwamba unaimarisha uhusiano huu.
Kuna uhusiano ambao wewe kama wewe unaweza kuanzisha. Na huu hapa, kuna kitu unaweza kufanya juu yake.

Katika makala haya ya siku hii ya leo nitaungumzia moja kwa moja uhusiano kwa wale ambao wanapenda kuoana au kuwa mme na mke. Na hapa sitazunguka sana, nataka nikwambie kitu kimoja tu ambacho  unapaswa kukiepuka kabla ya k uingia kwenye mahusiano haya.

Kama ambavyo nimetangulia kusema kwamba mahusiano ni sehemu ya maisha.  Na imekuwa kawaida vijana kujihusisha na mahusiano ya hapa na pale katika maisha ya kila siku.

Moja ya jambo ambalo limekuwa linawasukuma vijana walio wengi sana kuingia katika mahusiano ni kwa sababu rafiki yake kaingia katika mahusiano. Au mwingine kwa sababu anahisi mtu fulani atamwacha hivyo anapaswa kuharakisha ili huyo mtu asije akaoa au akaolewa na mtu mwingine. Wengine pia wamekuwa wakiingia kwenye mahusiano kwa sababu tu ya kulazimishwa na wazazi na ndugu baada ya kufanyiwa vikao. Wengine wamekuwa wanaogopa kwamba hapa miaka imeniacha hivyo napaswa kuingia kwenye mahusiano na kuoa au kuolewa.

Rafiki yangu kati ya kosa moja kubwa sana ambalo watu wanafanya ni kuingia kwenye mahusiano bila kuwa tayari. Hili ni  kosa kubwa sana ambalo wewe hupaswi kulifanya.

Haijalishi rafiki zako kiasi gani wameoa au wameolewa. Lakini je, wewe upo tayari kuingia katika mahusiano? Je, upo tayari kuyabeba majukumu ya kuwa baba au kuwa mama?

Haijalishi ndugu zako wamekaa vikao vingapi kukwabia kwamba sasa oa au olewa lakini je, wewe upo tayari kuingia kwenye hayo mahusiano?

Hili ni jambo muhimu sana ambao unapaswa kuhakikisha kwamba unalifahamu rafiki yangu kabla ya kuingia kwenye mahusiano.

Kuoa au kuoleawa sio FASHION. Kwamba sasa kuwa kuna fashioni hii ngoja nikimbizane nayo ikipita inakuja nyingine. My friend unahitaji kuhakikisha kwamba unakuwa makini sana. kwa wengine jambo hili linafanyika mara moja na kwa maisha yao yote. hivyo umakini wa hali ya juu sana unahitajika. Utayari wa wewe kulipokea jukumu hili na kulibeba ni muhimu sana.

Rafiki yangu, kwa leo naomba niishie hapo. Hivyo kama ulikuwa bado hujaingia wenye mahusiano, hakikisha unajihoji kwa umakini na kuangalia kama upo tayari au la. Kama hauko tayari ni bora ukasubiri mpaka utakapokuwa tayari.

NB. Usije ukatumia kigezo cha kutokuea tayari kama kigezo cha kukimbia majukumu. Hakikisha unaposema upo tayari uko tayari kweli. Unaposema haupo tayari haupo tayari kweli.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X