Kijana Usidanganyike, Wakati Unazidi Kusogea


Kumekuwepo na misemo kadha wa kadha ambayo vijana wamekuwa wakiitumia kujikinga wakati wanafanya jambo fulani.
Kwa mfano unakuta kijana anaangalia tamthiliya wakati wote, ukimuuliza kulikoni basi atakwambia maisha yenyewe menyewe magumu wacha nile ujana. Wakati huo huo anasahau kwamba muda anaosema anakula ujana  unazidi kusogea na hauji kujirudia kamwe. EBU KIJANA ANZA KUJIFIKIRIA MARA MBILI TATU HAPA.

Soma Zaidi: TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM; Hatua Sita (06) Za Kukutana Na Watu Maarufu,  Wafanyabiashara Wakubwa Na Wanamziki Nguri Bila Kutumia Nguvu

Kitu kimoja kikubwa ambacho vijana wamekuwa wakipoteza sana muda ni mahusiano yasiyo na mbele wala nyuma
Vijana wengi wamekuwa wakipoteza muda mwingi sana wakiingia katika mahusiano ambayo sio sahihi na pengine bila kupanga. Ukimuuluza kulikoni, basi atakwambia mimi NAPOTEZEA MUDA TU!!

Hapa nimegundua kwamba vijana wengi wanapoteza muda mwingi sana bila sababu za msingi.
Wakati msemo wa ninapotezea muda unazidi kupamba moto na kutumiwa sana miongoni mwa vijana, MUDA WENYEWE UNASONGA MBELE BILA HURUMA.

Inazidi kuwa asubuhi na inazidi kuwa jioni bila huruma. Wewe kijana unazidi kupoteza muda asubuhi mchana na jioni. Muda wenyewe haukusubiri.

Siku utakapokuja kuuhitaji muda basi muda wenyewe hautapata kamwe.

Nimejiuliza kwa kina sana, kwa nini vijana wanapenda kufanya vitu ambavyo sio sahihi kwa kisingizio cha ninapotezea muda?

Hapa nimegundua kwamba wanaosema napotezea muda sio tu hawana la kufanya bali hawajawahi hata siku moja moja kuwa watu wa kutunza muda na kufuata ratiba. Hivyo ni watu wa kupoteza muda siku zote.

Sasa hapa dawa ya huu ugonjwa ni ipi?
Mpaka hapo tushagundua ugonjwa uko wapi ila sasa dawa yake iko wapi?
Dawa yake inapatikana kwenye vitu hivi vifuatavyo

1. KIJANA KUWA NA MALENGO
Jijue wewe kama kijana ni wapi unaenda na kwa nini. Moja kati ya vitu vinavyonifanya nisisitize juu ya kuwa na malengo ni kwamba malengo muda wote yatakuweka kwenye mstari. Yatakuonesha ni wapi unapaswa kwenda na watu gani unapaswa kutembea nao. Malengo yatakuambia kwamba muda wako unapaswa kuuweka hapa, kwa kufanya jambo fulani na jambo fulani. Hivyo tu.

Kiukweli lazima niwe mkweli huwezi kumkuta kijana mwenye malengo anafanya vitu vidogo vidogo kwa kisingizio cha kwamba anapotezea muda. Hamna kitu kama hicho. Wale wote wanaofanya vitu kwa kupotezea muda, hawajui nj wapi wanaenda na kwa nini wanapaswa kwenda huko. Ndio maana wanakimbizana vitu vidogo sana kwa kisingizio cha ninapotezea muda.

Kijana usidanganyike, muda wenyewe haukusubiri. Hakuna muda wa kupoteza.

2. KIJANA IFANYE RATIBA YAKO IBANE SANA
Kinachowafanya vijana wakimbizane na vitu ambavyo sio vya msingi ni kutokana na ukweli kwamba ratiba za siku za vijana wengi ni ratiba ambazo hazina mpangilio. Kijana akiamka asubuhi mpaka anafika jioni anakuwa hana ratiba maalum kwamba leo nitafanya kitu fulani na nitafuatisha kitu kingine.

 Yaani kwake, kila kinachokuja mbele yake ni bora tu. Ndio maana usemi wa NAPOTEZEA MUDA unaingilia katikati.

Soma Zaidi:  Iko Wapi Motisha Januari Mosi?

Ukiwa na ratiba ambayo ina mwanya (gaps) mwingi ambapo utakuwa hufanyi kitu hapo ndipo utaanza kufanya vitu ambavyo sio vya msingi kwa kisingizio cha ninapotezea muda.

Kwa kijana hizi sio siku za kupoteza hata kidogo. Kuna maneno mazuri kwenye Kitabu cha Methali yanayotuasa vijana kuzitumia vyema siku za ujana kumkumbuka mwenyezi Mungu. Hata hivyo usemi huu haupaswi kuishia tu kwenye kumcha Mungu. Usemi huu tunapaswa pia kuutumia kwenye kazi. Siku za ujana ndizo siku muhimu sana, kwa kijana kuhakikisha amezitumia kwa kuchapa kazi. Kijana ibane sana ratiba yako ya ujana na fanya kazi nyingi sana maana zinakuja siku za uzee ambapo utatamani sana, sana kurudi kwenye ujana wako. Lakini pia haitaewezekana.

HITIMISHO
Kiukweli kwenye suala zima la kupotezea muda kama kila kijana  kuanzia leo atapotezea muda kwenye kufanya jambo la kujenga taifa. Basi taifa letu litajikwamua na kusonga mbele kwa kasi ya ajabu sana.

Lakini huu upotezaji wa muda wa kuangalia tamthiliya, kubeti, mapenzi, kuchati, kuzurura, kucheza kamari, n.k
Huu ni upotezaji kweli kweli. Narudia tena HUU NI UPOTEZAJI KWELI KWELI.

Kijana kama utendelea kupoteza muda wako kwa kufanya mambo unayoyafanya hayo, mimi sichelewi kusema uzeeni kwako UTAPATA TAABU SANA.

Ebu sasa badilika. Kwanza mimi nashangaa, unaanzaje kupata muda ambao unasema kwamba unapoteza.  Kama ulikuwa unautumia usemi huu sasa kuwa makini maana siku zenyewe hazigandi hata kidogo. Jana ndio imeshapita. Kesho ndio hiyo inakuja kwa kasi kubwa sana.

Kama baada ya hapa utapata muda tena wa kupotezea. Basi wewe bila shaka utakuwa haujaitwa kuwa makini kwenye dunia hii. Sikutishii ila nakwambia ukweli.

Namalizia kwa kusema hivi, kijana kuwa makini sana, muda wa kupotezea haupo. Usipovaa viatu vichafu ukiwa kijana utaluja kuramba vumbi uzeeni mwako.

Kijana usidanganyike, wakati unazidi kusogea.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA NA UJAZE TAARIFA ZAKO


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X