Kitu Chochote Ambacho Hakikuumizi, Kinakuimarisha


Hongera sana rafiki kwa siku hii ya leo.
Kama kuna kitu kikubwa sana ambacho unapaswa kufanya ndani ya siku hii ya leo basi ni kukua. Kwenda ambapo ulikuwa hujawahi kwenda. kuuza kitu katika biashara yako kwa mtu ambaye ulikuwa hujawahi kumuuzia. Kuongeza kipato chako leo ili kiwe tofauti na kilivyokuwa jana.

Kuongea na mtu mmoja ambaye anakuhamasisha zaidi maishani.

Kwa hakika leo ni leo. Wala usiseme kesho. Kama unapaswa kufanya kitu leo. Basi kifanye leo.

Yote hayo unayoyapanga kuyafanya leo, hayatatokea tu kirahisi rahisi. Yaani kwamba unampiga simu na kumwambia juu ya bidhaa yako, au juu ya mzigo mpya uliouingiza kwenye biashara na yeye anaamka papo hapo kuja kununua?

Hasha! Kiukweli ni kwamba wapo watu watakaokataa, na kusema HAPANA. Hapo sasa ndipo wewe unapaswa kuiona hiyo kama fursa ya wewe kuendelea kuongea nao.

Wapo leo watakuona unaweka juhudi kubwa sana kuhakikisha kwamba unatimiza malengo yako, watasema kwamba HUWEZI, hapo sasa ndipo unapaswa kuendelea na motisha yako ya kusonga mbele na kuhakikisha kwamba unasonga mbele zaidi.

Soma zaidi:  Hii Ni Siku Unayopaswa Kuiishi

Maana kama watu hawa hawakuumizi sehemu yoyote ya mwili basi wana nia ya kukuimarisha.  Kiufupi naweza kusema kwamba wale watakaokukatisha tamaa wanataka usonge mbele, kwa hiyo wewe usiache kufanya. Bali ongeza spidi, motisha na tenda kazi mara kumi zaidi ya hapo, huku ukifahamu kama hawakuumizi basi wanakufanya usonge mbele.

Hii inapaswa kuwa kanuni yako ya maisha. Kila siku ya maisha yako na kila hatua yoyote utakayochukua, fahamu kwamba kila anayeongea kitu, au kufanya kitu kwa lengo la kukutatisha tamaa. Basi kama mtu huyo hajakuumiza sehemu yoyote ya mwili wako (au kiufupi niseme, hujapata jeraha kutokana na kitendo chake), basi jua mtu huyo anakuimarisha.

Kwa namna yoyote usikubali kirahisi kukata tamaa. Weka juhudi, nguvu huku ukifahamu kwamba KITU CHOCHOTE KILE AMBACHO HAKIKUUMIZI BASI KINAKUIMARISHA.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X