Kitu Kimoja Ambacho Unapaswa Kukiepuka


Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii njema sana ya leo. Binafsi nafurahi sana maana siku hii ya leo ni siku ya kipekee sana katika maisha yetu na kama kawaida hakikisha unaweka juhudi kubwa sana katika kuhakikisha kwamba unazidi kusonga mbele.

Rafiki yangu siku ya leo kwako iwe ya kivitendo zaidi kuliko maneno.

 Hakikisha kwamba unaweka kazi pale inapopaswa kuwa siku hii ya leo na maneno yanakaa yanapopaswa kukaa. Haitoshi tu wewe kuwa muongeaji ndani ya siku hii njema ya leo. Utaipoteza siku yako.

Hivyo fanya, na hakikisha unafanya. Na fanya kweli, hakuna jinsi ambavyo siku hii ya leo unaweza kuona umefanya cha maana  sana kama utakuwa muongeaji badala ya mtendaji.

Rafiki yangu nomba nikwambie kitu. Siku hii itumie kuongea kidogo sana, ila wakati huohuo fanya kazi sana.
Matendo kwako ndio yanapaswa kuongea sana kuliko maneno.

Katika kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI nimekushirikisha maneno mawili muhimu  sana unayopaswa kuyatumia wakati wa kazi ili kuepuka kuwa mtu wa maneno mengi sana. Unaweza kuyatumia maneno haya badala ya kuwa muongeaji na ukajikuta unapata muda zaidi na zaidi.

Na maneno haya sio mengine, bali ni maneno
Asante na Thanks.

Maneno haya yatakupunguzia mamilioni ya sentensi ambazo utaziongea kwa siku na kujikuta unapata muda zaidi na zaidi wa kufanya kazi kwa siku husika.

Rafiki nakuomba kitu kimoja siku ya leo ukifanyie kazi. Basi leo kafanye matendo. Nashukuru sana rafiki kwa kuweza kusoma mpaka mwisho.

Mwisho nakuomba ukawe na siku bora kwa kuweka katika matendo kile ulichosoma hapa. Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X