Kitu Kimoja Cha Thamani Unachoweza Kufanya Siku Yako Inapoanza


Kwa kawaida sana asubuhi watu huwa wanakimbizana na vitu vingi sana, sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu walio wengi huwa wanaianza siku wakiwa wamechelewa hivyo kujikuta wamechelewa kufanya baadhi ya vitu. Na hivyo kuna vitu ambavyo watu huwa wanasahau kabisa kuvifanya.

Soma Zaidi: Nani Ametengeneza Kanuni Hii? Haifanyi Kazi!!

Kuna vitu vingi unaweza kufanya asubuhi ila jambo moja hili ni muhimu sana, sana. Na jambo hili sio jingine bali ni kupangilia siku yako. Ukiweza kuipangilia siku yako unapoamka asubuhi vizuri, kwa hakika utakuwa na siku bora sana. Maana utaishi ndani ya siku yako kwa viwango unavyostahili kuishi. Utafanya kile ambacho unapaswa kufanya ndani ya siku yako. Lakini pia utaepuka kile ambacho hukupaswa kufanya.

Rafiki yangu,  Kitu kimoja cha thamani unachoweza kukifanya siku yako inapoanza ni kupangilia siku yako.

Kama rafiki yangu tabia hii hauna wala hujawahi kuwa nayo sasa ni muda wako wa kuhakikisha kwamba unaianzisha.

Tabia hii itakuongezea muda wa ziada kwa siku yako na itakufanya ufanye kazi ambazo ni za muhimu sana kwako.

Rafiki yangu ianzishe tabia hii muhimu sana.

Soma Zaidi: JE, UNAAMKA SAA NGAPI? JE,UNAFANYA NINI BAADA YA KUAMKA? Mbinu Mpya Na Zilizothibitishwa, Zitakazokuwezesha Kuamka Asubuhi Na Mapema

MUDA WA ZIADA; Sehemu Moja Muhimu Unayoweza Kupata Muda Wa Kufanya Kazi Zako Tofauti Na Ajira

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X