Kwa kawaida mawasikiano kati ya mtu mmoja na mwingine yanapitia katika lugha. Lugha ndio kiunganishi kati ya watu wa mataifa, na makabila mbali mbali.
Kwa Tanzania Kiswahili ndio lugha yetu ya taifa ambayo inatuunganisha sana. Kwa sasa hivi ukienda kwenye kila kona ya Tanzania basi utakuta watu wanaongea Kiswahili. Hata kama bado utawakuta watu hao wanaongea lugha nyingine, bado ukiongea Kiswahili utaeleweka na utaweza kuhudumuwa.
Kiingereza ndio lugha inayotutambulisha kimataifa. Sasa hivi walau kila mzazi anajitahidi kuhakikisha mtoto wake anaijua lugha hii. Na pengine mzazi mwenyewe anahakikisha anaifahamu lugha hii. Yote haya ni kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano.
Soma Zaidi: Jifunze Mawasiliano
Sasa kama kawaida yangu leo nataka utafakari suala zima la lugha kutokea kwenye kona nyingine kabisa! Tunaanza.
Hivi ushawahi kujiuliza maisha bila lugha ya kawaida ya maneno yangekuwaje? Au kujiuliza kama inatokea sasa hivi unaenda sehemu ambapo hawajui lugha yako na wewe hujui lugha yako utaishije? Utaombaje maji? Utapaje chakula?
Je, kuna lugha nyingine ambayo inaweza kukuunganisha wewe na watu wengine bila kuongea.
Jibu langu ni ndio. Na lugha hii sio nyingine bali ni lugha ya mwili. Mwili wa binadamu unaongea zaidi ya meneno. Wanasaikolojia wanasema lugha ya mwili huchangia takribani asilimia 70 ya maongezi kati ya mtu mmoja na mwingine.
Lugha ya mwili inaweza kukwambia kwamba mtu fulani amekupokea au hajakupokea.
Lugha ya mwili inaweza kukwambia kwamba mtu fulani anafurahia uwepo wako au hafurahii uwepo wako.
Lugha hii hutokea bila mtu mwenyewe kujua na hivyo wewe kujikuta unapata kujua mengi kuhusu mtu huyo ambaye unaye kuliko mtu mwingine yeyote. Rafiki yangu, kama lugha ambazo utapaswa kujifunza, kuzijua na kuziishi basi ni lugha ya mwili.
Kwangu sasa unakarbia mwaka tangu nilipoanza kuisoma na kuifutilia lugha ya mwili. Ukisona na kuielewa lugha ya mwili utafurahia mambo mengi saba ambayo mtu anashindwa kukwambia kwa mdomo. Au mtu anayasema kwa mdomo kwa uongo. Yote haya utapata kuyajua kupitia lugha ya mwili.
Rafiki yangu, nakushauri sana sana, usikose kuifuatlia lugha ya mwili kuanzia sasa.
Na binafsi nitakuelekeza kitabu kimoja muhimu sana ambacho ukikisoma na kuyaishi yote yaliyoandikwa mle juu ya lugha ya mwili utafurahia sana. Kitabu hiki sio kingine bali ni kutabu cha KILE AMBACHO KILA MWILI UNAONGEA. Kitabu hiki kwa kiingereza kinaitwa WHAT EVERY BODY IS SAYING. Kimeandikwa na Joe Navarro.
Ni kitabu kizuri, kizuri sana. Kama unahitaji kuwajua watu waliokuzunguka, kuwasoma watu waliokuznguka basi soma kitabu hiki hapa.
Rafiki yangu kitabu hiki kama unakihitaji kinapatikana kwa mfumo wa soft copy na nitakutumia buree kabisa kwa njia ya email. Unachohitaji ni wewe kunitumia email yenye neno KITABU CHA LUGHA YA MWILI kwenda godiusrweyongeza1@gma.com
Utapokea kitabu na utaanza kusoma ili upate maarifa haya. Kumbuka kwamba Kitabu hiki ni cha kiingereza, sio kiswahili.
Karibu sana
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391