Sifa Tatu Wanazobeba Wajasiliamali Kwa Pamoja


Kuanzisha, kukuza na kuendeleza biashara kuanzia chini sio suala la kuchukulia lelemama. Ni suala ambalo kiukweli lina misingi yake mikubwa sana ambayo ipo na misingi hii wajasiliamali makini sana wanaifahamu.  Na ukiwafuatilia watu wote walioanzisha na kukuza biashara zao basi utaguandua kwamba kuna vitu ambavyo wao wanavyo, vinavyowaunganisha na kuwafanya wazidi kung’0aa na kuinua biashara zao.

Sasa siku ya leo nimekuandalia mambo matatu ambayo yanawaunganisha wajasiliamali wote kwa ujumla.

1. WAJASILIAMALI NI WATU WENYE MALENGO
Mjasiliamali kwa kawaida ni mtu ambaye anajua anaenda wapi. Anataka kufanya nini na kwa nini anataka kufanya kile kitu.

2. WAJASILIAMALI HUTENGENEZA BAHATI
Mara nyingi watu wakimwona mtu aliyefanikiwa basi hapo hapo huwa wanasema jamaa huyu ana bahati. pengine huwa wanaanza kukisia na kusema vitu ambavyo sio kweli. Ni wakati huu huu ambapo utasikia watu wakisema kwamba “jamaa huyu aligusa tu mambo yakatiki”. mwingine utasikia anasema “jamaa huyu ni freemason”. Na mwingine atadiriki kusema kwamba “huyu jamaa alibahatika kupata mtaji kutoka kwa baba au mama la sivyo angekuwa na maisha ya hali ya chini sana” . Ila mimi ninachofahamu juu ya watu waliofanikiwa ni kwamba ni watu ambao wanatengeneza bahati. Na bahati zao huzitengeneza kwa matendo. Yaani matumizi yake ya pesa, uwekezaji anaoufanya, akiba anazoweka vyote hivi huwa na hivi kwa pamoja humfanya atengeneze bahati.

Soma Zaidi: KITABU: NYUMA YA USHINDI

3. KUFANYA KAZI KWA BIDII
Moja ya sifa nzuri sana ya wajasiliamali wote ni kufanya kazi kwa kujituma sana. Tupo katika zama ambapo watu wengi sana hawapendi sana kusikia neno kazi. Ndio maana utasikia watu wanasema kwamba mimi napenda nifanye kazi ambayo haina stress. Wakimaanisha kwamba hawapendi kujisumbua kwa kazi ngumu na inayofanyika muda mrefu sana.  Sasa wajasiliamali wanaiona hii kama fursa kwao na kuhakikisha kwamba wanaitumia. Wao wapo tayari kufanya kazi kwa muda kujituma, na kwa muda mrefu sana. Na wewe unaweza kuiga hapa

Soma zaidi: Huu Ni Ubishi Ambao Kila Mtu Anapaswa Kuwa Nao

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X