Swali Moja Ambalo Kila Mwenye Malengo Anapaswa Kujiuliza Kila Wakati


Kuna maswali ya kila aina ambayo unapaswa kujiuliza kila siku unapoamka asubuhi, mchana na jioni haswa linapokuja suala zima la kuelea kwenye kilele cha malengo yako.

Soma Zaidi: Maswali Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Kila Unapoamka Asubuhi

Soma Zaidi:  Maswali Muhimu Ya Kujiuliza Kabla Ya Kuingia Kwenye Ujasiliamali

Ila kiukweli kuna swali moja muhimu sana ambalo unapaswa kujiuliza wakati unafanya kazi yoyote. Iwe unatembea, iwe unacheza au unaongea na mtu.

Na swali hili sio jingine, je, mtu ambaye ni bora sana kwenye hiki kitu sasa hivi anafanya nini?

Jibu la swali hili litakufanya ujisukume zaidi. Ukishajua mtu ambaye ni bora zaidi duniani yupo anafanya nini basi na wewe utaongeza juhudi ili ufanye bora.

Unapaswa pia kujiuliza je, kama mimi ningekuwa ndiye mtu anayetegemewa sana duniani na mimi ndiye mtu bora sasa hivi ningekuwa nafanya hiki ninachokifanya?

Ukiona hakifai, basi achana nacho  kafanye kitu kingine ambacho unaona wewe kama mtu bora sana duniani unapaswa kuwa unafanya.

Hivi ndivyo unavyoweza kujiuliza maswali ya kukusukuma kufikia ndoto zako.

Soma Zaidi: Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini-3

Hawa Ni Watu Watano Ambao Unapaswa Kuwasikiliza

Asante sana,

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X