TWO IN ONE: Jinsi Ya Kutumia Kanuni Hizi Mbili Kama Kitu Kimoja.


Siku zote  mtu kama unapenda kupata kitu kikubwa sana, lazima uwe tayari kuchukua hatua kubwa sana.

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini leo hii nimeanza na kauli kama hiyo hapo. Ni kweli rafiki yangu, lazima ujiulize. Najua kwamba katika maisha unataka kupiga hatua kubwa sana ya kukutoa hapo mpaka viwango vingine vya juu kabisa.

Na ili uweze kufikia viwango hivyo, basi huna budi kuchukua hatua madhubuti. Mimi naziita HATUA KUBWA SANA. Sio hatua za kawaida ambazo kila mtu anachukua.

Ninasema hivi kwa sababu kuna wakati mfano ndoto yako itawahitaji watu, utahitaji watu walio mbele yako ili waweze kukusogeza na kukuvuta wewe hapo ili uingie kwenye viwango vingine. Unajua nini?

Watu hawa hawatakuwa tayari?  Sio kwamba hawapo tayari kwa sababu hawakujali, au kwa sababu hawapendi ndoto zako. Ila hawapo tayari kwa sababu, NA WAO WAPO BIZE, NA WANA KAZI NYINGI SANA ZA KUFANYA.

Soma zaidi: TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM; Hatua Sita (06) Za Kukutana Na Watu Maarufu, Wafanyabiashara Wakubwa Na Wanamziki Nguri Bila Kutumia Nguvu

Hivyo mpaka waanze kukufikiria wewe mtu unayejitokeza hivi hivi tu mbele yao, haitakuwa rahisi. Kwa sababu hiyo wewe hapo utapaswa sasa kuchukua HATUA KUBWA na KUWA MSUMBUFU.

Ndio unapaswa unapaswa kuwa msumbufu. Wakumbushe kila mara juu ya ndoto zako. Wakumbushe kwamba unategemea kitu fulani kutoka kwao,
Wakumbushe kila mara kwamba unapenda kuungana nao katika biashara wanazofanya,
Wakumbushe kwamba unawahitaji kama wateja wa bidhaa zako.

Hakika, kwa namna hii rafiki yangu utafurahi sana sana. Mwisho wa siku utashaangaa wanakubali. Pengine wanaweza wasiwe wamekubali kama kukubali, ila wakawa wamekubali kama ishara ya kupunguza usumbufu wako.

Unaona rafiki yangu. Hatua kubwa inafanya kazi. Wao wanapunguza usumbufu, wewe unapata fursa ya kuonesha kile ulichokuwa unataka kuonesha. Wao wanapunguza usumbufu, wewe unapata nafasi ya kuonesha kipaji chako, wewe unapata nafasi ya kuuza bidhaa yako, wewe unapata nafasi ya kuongea kwenye redio.

Kumbe usumbufu unalipa. Sasa ngoja nikwambie kitu kingine kuhusu USUMBUFU na HATUA KUBWA.

 Unapopata nafasi hii itumie vizuri kweli kweli kiasi kwamba hata siku nyingine watakuwa tayari kukutafuta na kuongea na wewe tena. Itumie vyema nafasi hii kiasi kwamba siku nyingine watakuwa tayari kukutafuta na kununua kitu kutoka kwako.

Rafiki yangu, yangu kanuni mbili zilizounganishwa kuwa kitu kimoja nilizotaka kukuwambia leo hii ni
1. HATUA KUBWA
Kama ambavyo uneona tangu mwanzo mwa makala haya, nilikuwa nakusisitizia wewe juu ya kuhakikisha unachukua hatua kubwa kila siku na kwenye kila jambo.
2. USUMBUFU
Lakini pia hatua hizo kubwa sana zinapaswa kuendana na usumbufu. Unapaswa kuwa msumbufu, msumbufu kweli kwenye kile unachofanya mpaka kieleweke.

Soma zaidi : Aina Tatu (03) Za Watu: MOTO, BARIDI NA UVUGUVUGU

Rafili yangu, hizo ni kanuni mbili ambazo unaweza kuziunganusha kuwa kitu kimoja.

 Asante sana sana rafiki yangu. Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X