Uchambuzi wa Kitabu: FAILING FORWARD Ukianguka angukia mbele


Hivi ni kitu gani kinawafanya watu wengine wanafanikiwa na wengine wanashindwa. Je, ni kitu gani kinawafanya watu wengine wanaonekana kila wanachogusa kinabadilika kuwa dhahabu huku wengine wanaonekana  kila wagusacho haking’ai. Je, inaweza kuwa ni familia ambazo watu wamezaliwa? Hapana maana watu wawili wanaweza kuwa wamezaliwa kwenye familia moja, mmoja akatokea kuwa mwenye mafanikio na mwingne akaishi maisha yake yote kwa kubangaiza.

Je, ni kiwango cha elimu? Na hili hapana pia maana kuna watu wengi sana ambao wana visomo vikubwa ila bado hawajaweza kufanikiwa kabisa kwenye maisha. Je  nini hiki kinawafanya baadhi ya watu kufanikiwa na wengine kupita katika maisha yao?

 Je, ni kushindwa?
Ndio ni kushindwa. Hii ndio tofauti kubwa na ndipo ulipolala utofauti kati ya watu waliofikia mafanikio na wale ambao hawajafanikiwa. Watu waliofanikiwa wanajua kwamba wao wakishindwa, au wakianguka basi wanapaswa kuangukia uso. Lakini watu wa kawaida wakiainguka wao wanaanguka mwanguko wa mende.

Mwandishi JOHN C. MAXWELL ametushirikisha hatua 15 za watu waliofanikiwa kwa kushindwa na kututaka na sisi tuweze kuzitumia siri hizi kwa maufaa yetu ili hatimaye tuweze kufikia kwenye kilele cha mafanikio. Katika makala haya tunaenda kuzungumzia kuona hatua tano za mwanzo. Na hatua hizi hapa ni kama ifuatavyo.

HATUA YA KWANZA; IFAHAMU  MOJA KATI YA WATU WA KAWAIDA NA WATU WALIOFANIKIWA.

1. Je, ukiulizwa kitu kimoja kinachowatofautisha watu walioanikiwa na watu wambao hawajafanikiwa utasema nini? Kitu hiki hapa bila kupepesa macho ni kushindwa. Hapa kuna vitu saba ambavyo unapaswa kuvifahamu kuhusu kushindwa.

2. Kushindwa hakuepukiki

3. Kushindwa hakutokei kama.magonjwa ya mlipuko . Ukishindwa haushindwi mara hiyo, ni mchakato. Chukullia mfano wa kushindwa mtihani, sio kwamba unashindwa kwenye chumba cha mtihani, hapana ni chakato tokea nyuma

4. Kushindwa kwako huwezi kukugeuzia kwa mwingine

5. Kushindwa sio adui. Hata katika hali hatari kushindwa ni rafiki

6. Sio kweli kwamba kushindwa hakubadilishwi.

7. Kushindwa kama alama ya kudumu. Ukishindwa angalia kiilichokufanya kushindwa baada ya hapo songa mbele. Endelea kufanyia kazi kile ambacho unaona ulikosa na songa mbele.
Kushindwa sio mwisho.
Kwa hiyo hakikisha kila siku unafanya kitu cha kukufanya wewe uweze kusonga mbele.

 8. katika dunia hii watu wengi sana waliweza kufikia mafanikio makubwa sana ni watu waliokutana na kushindwa katika njia nyingi sana. akina Thomas Edison walishindwa mara nyingi sana. hata mitume, akiwepo Paulo walishindwa ila hawakuwahi kuona kushidwa kama mwisho. Badala yake waliona kama mchakato wa wao kujifunza na kusonga mbele.

HATUA YA PILI; . MAANA MPYA YA KUSHINDWA NA MAFANIKIO

9. hapo juu tumeona vitu saba kuhusu kushindwa lakini hatujaona maana halisi ya kushindwa., Sasa kushindwa ni nini? KUSHINDWA NI GHARAMA TUNAYOLIPA ILI KUFIKIA MAFANIKIO.

10. Kwa hiyo kila mara tunapokutana na kitu ambacho tunafanya na kile kitu kinaonekana kwamba  tumefanya na hakijafanikiwa, badala ya kusema kwamba tumeshindwa. Jiambie kwamba  mbinu niliyotumia ndio haijafanya kazi. Hata siku moja usiruhusu wewe kujiona kama mshindwa.

11. Kinachowatofautisha washindi na wengine ni kwamba washindi kila mara huweka akili yao kwenye kushinda.

12. Washindi wanadunda. Wakianguka chini hawajishikilii hapo hapo, badala yake wanadunda na kusonga mbele.

HATUA YA TATU,
JITOE KWENYE KUSHINDWA.

 13. Acha kuujaza ubongo wako kila mara na mambo hasi yanaoonesha kwamba wewe huwezi kufanya kitu kikubwa sana. badala yake weka akili yako mara kwa mara kwenye kuona picha kubwa ya wewe na mafanikio.

HATUA YA NNE,
CHUKUA HATUA NA JIONDOE KWEYE KUSHINDWA.

14.  Kuna vitu vinafanya watu waendelee kushindwa kila mara uoga, kutochukua hatua, kutokuwa na ujuzi, kutokuwa na uwezo . na vitu hivi hutengeneza mzunguko. Kwa kuwa watu wengi wanajikuta hawana hivi vitu basi kila mara utawakuta wanalalamika bila kuchukua hatua. Mwisho wa siku wanabaki humu kwenye huu mzunguko bila kwenda mbele. Sasa ili uweze kusoga mbele unapaswa kuuvunja mzunguko huu. Ni uamuzi wako kuamua kuuvunjia wapi  na kuanza kusonga mbele kama vile hakuna kitu chochote kinachokuzuia.

15. Mzunguko wa kushundwa unaweza kuuvunjia popote. Unaweza kuamua kuanza kuondokana na uoga au kutafuta ujuzi. Ilimradi uwe tayari kuchukua hatua kuondokana na hali hii.

16. Badilisha mtazamo wako wa kushindwa kwa kukubali majukumu.

17. Unapaswa kujiuliza kwa nini unafanya kitu fulani. Sio tu kwa sababu umekuta wazai au watu fulani wanafanya kitu fulani na wewe unafanya vilei vile. Au kwa sababu tu  umekuta watu wanasema kwamba hawawezi kufanya kitu fulani basi na wewe unaona kwamba sasa hapa kweli siwezi kufanya. Hapana,  mambo hayako hivyo
Kama utaendele kufanya mambo katika namna ile ile kila siku utaendelea kupata matokeo yale yale. Kwa hiyo badili, mtazamo wako.

18. Amka na tafuta sehemu ya kutokea. Hii ndio njia pekee ya wewe kuondokana na kushindwa.

Yafanyie kazi haya rafiki yangu,

Asante tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X