Kila mtu katika maisha anapenda kuwa na mahusiano mazuri. Anapenda kuolewa au kuoa mke ambaye wataweza kuishi kwa pamoja na kufurahia maisha.
Hata hivyo wanandoa walio wengi huwa wanaishia kulia, hii ni kutokana na ukweli kwamba mambo waliyokuwa awanayategemea kukutana nayo kwenye ndoa huwa yanakuwa kinyume kabisa. Pengine mwenza waliyekuwa wanamwamini kwamba huyu ndiye, hugeuka kuwa mwiba na kuwachoma na wao kuumia sana.
Haya yote yanatokea kutokana na ukweli kwamba vijana walio wengi wakiingia kwenye mahusiano wanaingia kichwa na miguu. Hivyo hawataki kuwahoji wa kuwauliza maswali wenza wao, wakidhani kwamba watawaudhi na kuwapoteza. Na pengine ni kwa sababu maswali haya hayaamushi hisia za kimapenzi basi vijana wengi hawapendi kuyauliza ila wanakimbilia kufanya vitu ambavyo vinaamsha hisia za kimapenzi.
Mwandishi wa kitabu cha 101 QUESTIONS TO ASK BEFORE YOU GET ENGAGED ambaye ni H. Norman Wright anasema mahusiano mazuri au mabaya yanaonekana mapema kabla ya ndoa.
Mwandishi huyu anatuambia kama.kuna kitu katika mahusiano yenu unaona kabisa kwamba hakiendi vizuri basi usikae na kuanza kusema nikioa au nikiolewa kitakaa vyema. Wewe sio kiwanda cha kubadili watu. Kwa hiyo kitu chochote ambacho kabisaa unaona hakiendi vizuri usiruhusu kiendelee kuwa hiyo. Hoji. Kama mwenza hatakupa majibu ya kukuridhisha basi achana naye. Ndio ACHANA NAYE.
Mwandishi anasisitiza kosa ambalo hupaswi kufanya kwenye maisha ni kuchagua mtu wa kuishi naye. Mwandishi anahoji kwa kuuliza ni nani anaweza kufanya ujinga wa kwenda kununua gari lolote bila kuuliza? Yaani kwamba yeye anafika tu eneo la magari na kusema nimelipenda gari hilo, basi niambie bei nilipe niondoke. Bila hata kuuliza swali!
Lakini watu walio wengi wanajikuta wanafanya hivi. Yaani wananunua magari (wanaoa au kuolewa) bila kujua gari hilo kwa undani.
Karibu sana rafiki katika maswali haya 101 ambayo unapaswa kumuuliza mwenza wako kabla ya kumvisha pete.
Kumbuka kwamba maswali haya hayavutii kuuliza, hayaamushi hisia za kimapenzi na pengine yanaogopesha kuuliza ila ni muhimu sana, sana kuuulizwa kwa mtu ambaye unataka kuwa naye maisha yako yote.
Kila utakapopata majibu yatunze katika akili yako ili baada ya muda uje umuulize tena ujue kama bado msimamo wake ni ule ule au umebadilika.
4. Elezea jinsi ulivyolelewa kama mtoto. Je, ukipata watoto utawalea kama ulivyolelewa kipindi ukiwa mtoto?
Je, kuna utofauti kati ya malezi aliyoyapata yeye na ambayo umepata wewe? Na je, utarahia jinsi ambavyo anaenda kuwalea watoto?
5. Je, ni sababu gani tano zinakufanya wewe utake kuishi na mimi maisha yangu yote? Na ni sababu gani zinakufanya usipende kuishi na mimi maiaha yangu yote.
Hakikisha anajibu maswali yote hayo mawili. Kama ataweza kujibu sababu za kwa nini anapenda kuishi na wewe huku akisema hana sababu za kutoishi na wewe, basi hapo unapaswa kuwa makini.
6. Kitu gani umajifunza kutoka kwenye mahusiano yaliyopita ambacho kitakufanya kuwa mwenza mzuri wa mtu sasa hivi?
Kila mahusiano huwa ni somo. Na kwa baadhi ya watu huwafanya kuwa wenye busara huku wengine huwafanya waondokewe na hekima. Usiingie kwenye mahusiano na kutoka tu kama.unavyoingia chooni na kutoka. Jifunze kitu kitakachokufanya kuwa mtu bora zaidi. Na pale utakapoingia kwenye mahusiano mapya basi kuwa tayari kumshirikisha mwenza wako mpya jambo ulilojifunza kutoka kwenye mahusiano ya nyuma.
7. Elezea safari yako ya kiroho kwa miaka kumi iliyopita. Hapa unapaswa kuhusisha sehemu ambazo ulikuwa unafanya vizuri na vibaya kwenye kipindi chote.
Yawezekana wengi hawajawahi kujiuliza maswali haya au kutafakari safari ya kiroho kwa miaka kumi. Lakini jambo hili ni muhimu sana kukifamu.
8. Ni kumbukumbu gani tatu muhimu unazikumbuka tangu ukiwa mtoto mpaka unafikisha miaka 18?
Iwe zilikuwa chanya au hasi, je, ni watu gani walihusika kwenye kumbukumbu hizi?
9. Je, neno kuendana kwako linamaanisha nini?
10. Je, kiwango cha mawaailiano yenu mnakionaje? Na je, usemi wa ongea lugha ya mwenza wako unauelewaje?
Kabla ya mahusiano kila mtu huwa anaongea lugha yake. Kipindi cha mahusiano kuna watu huwa wanaficha baadhi ya vitu, wengine wanaviongeza vinakuwa zaidi na wengine wanavipunguza kabisa. Ila yote kwa yote hapa hakuna mbaya au anayekosea. Ila mwenza mzuri ni yule anayeweza kuongea lugha ya mwenza wake.
11. Utakapooa au kuolewa utapaswa kujitegemea na kusahau juu ya msaada wa wazazi. Je, upo tayari kuwaacha? Je, kitu gani kitakuumiza na utakikosa kutoka kwa wazazi? Je, upo tayari kuishi mbali na wazazi?
12. Je, ni rahisi kwako kukaa na mtu ambaye mpo kwenye mahusiano na kusali?
Sala ni kiunganishi kikubwa sana kati ya watu na Mungu. Kama mtu ni mkweli kwa Mungu wake, basi hawezi kuwa mwongo kwa mwenza wake. Lakinj pia huwaunganisha watu zaidi badala ya kuwatenganisha.
13. Je, ni kwa kiwango gani wewe ni mtumiaji au mwekaji wa akiba? Haoa kinachozungumziwa ni pesa tu.
Kama wewe ni mtumiaji ni kiwango gani? Na kama ni mwekaji wa akiba ni kiwango gani?
Na je, utawezaje kuishi na mtumiaji kama wewe ni mwekaji akiba au kinyume chake?
15. Elezea maisha yako yalivyokuwa kabla hujakutana na Mwenza wako.
Unapokuwa na mwenza lazima baadhi ya mambo yatabadilika tu. Mengine ni chanya na mengine ni hasi. Wenzako wakisema siku hizi baada ya kukutana na fulani umebadilika. Basi hapo unapaswa kutafuta ni kitu gani wanamaanisha.
16. Ndoto kwenye mahusiano ni muhimu sana. Sasa mwambie mwenza wako aandike na kukamilisha sentensi hii mara kumi
Kama nitaoa/nitaolewa nitafanya…..
17. Ni maswali gani kuhusu mimi siku zote umekuwa unapenda kuniuliza ila hujawahi kuniuliza?
Hapa utashangaa sana. Maswali ambayo hukutegemea yatakuja. Mwenza wako akikuuliza maswali ambayo yanakugusa sana usihamaki. Tulia na hakikisha unajibu maswali haya kwa undani haswa. Kama swali linakuhitaji wewe kufikiria, basi usisite kumwambia akupe muda kidogo.
18. Unafikiri kusudi la Mungu kwenye mahusiano ni lipi?
22. Kama ningekuwa daktari na wewe ni mgonjwa unaniambia historia yako kiafya, ingehusisha nini?
Wengi sana wameshangaa kuja kujua kwamba mweza wao ana ugonjwa fulani baada ya kuoana. Kitu ambacho wamehukulia kwamba wamedanganywa.
23. Kama kuna kitu kimekuudhi juu yangu utatumia njia gani kuniambia.
28. Ni tabia gani unafurahi kuwa nazo na tabia gani unatamani usingekuwa nazo.
Kila mtu ana tabia zake. Je,unajisikiaje kuhusu taia za mwenza wako? Je, upo tayari kuendana nazo?
31. Miaka kumi kutoka sasa, unapenda kuwa wapi kiuchumi,kuroho na kifamilia?
Rafiki, maswali haya yapo 101. Nakushauri uchukue kitabu hiki ukisome mwanzo mpaka mwisho. Utapata kujifunza mengi, mengi sana.
Leo hii nimekushirikisha maswali machache kati ya hayo 101.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
One response to “UCHAMBUZI WA KITABU: Maswali 101 Ya Kumuuliza Mwenza Wako Kabla Ya Ndoa”
Nimepata mbinu mpya๐๐๐๐