UCHAMBUZI WA KITABU: THE ALCHEMIST


Ukisia watu hawasomi vitabu, basi jua kwamba hawasomi kwa sababu ya uzembe. Ukisikia watu wanasoma vitabu jua kwamba wamejitoa kweli kutafuta maarifa  na wana kiu ya maarifa.

 Katika dunia hii unaweza ukaamua kufanya kimoja kati ya hayo hapo. Mosi kujitoa au kuzembea. Na huwezi kufanya yote mawili.

Kwa nini nimeanza uchambuzi wa leo kwa namna hii. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi siku zote wanasema hawasomi vitabu kwa sababu vitabu ni vikubwa sana. Mfano rafiki yangu mmoja aliniambia TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA  kina kurasa 218, hivyo ni kikubwa hawezi kukisoma. Lakini bado kuna  vitabu vidogo sana, ila watu hawavisomi. Na kitabu hiki sio kingine bali ni THE ALCHEMIST ambacho nimeweza kukisoma kwa siku moja tu.

Kitabu hiki nimekipata kwa rafiki yangu mmoja ambaye najivunia kuwa naye, alinishirikisha kitabu hiki cha the ALCHEMIST mnamo mwezi wa nne. Baada ya hapo akaniasa nikisome. Nilikuwa tayari nimepangilia ratiba yangu usomaji na nikawa nimekiweka kwenye orodha ya vitabu muhimu vya kusoma siku za mbeleni. Sasa leo hii. Nimekisoma na kukimaliza. Hakika nimepata kujifunza mengi sana kutoka kwenye kitabu hiki hapa.

Karibu sana tujifunze kwa pamoja mambo 21 ambayo nimeyapata kwenye kitabu hiki hapa.

1.  Watu wengi sana wana mipango na ndoto kubwa sana. Ni wachache sana wanaochukua hatua wanaoweza kuifikia.

2. . Kile kitu ambacho watu wanafikiri juu yako kinakuwa na madhara kwao na sio kwa kwako.

3. Vitu ulivyonavyo, vinaweza kukufanya uzione fursa au usizione kabisa.

4. Ukiona mtu anasema LEO KAMA JANA TU! basi hapo unapaswa kufahamu wazi wazi kwamba mtu huyu anashindwa kuziona fursa zilizomzunguka, anaishi tu ilimradi anaishi, anavuta pumzi ilimradi kavuta pumzi.

5. Ushauri ni muhimu kwako wewe unapoelekea kwenye ndoto yako. Na katika kutafuta ushauri watafute washauri waliobobea kwenye sekta husika.
Kuna wakati utapaswa kulipia ushauri huo, hata kama mtoa ushauri atakushauri mambo machache sana.

6. Kama katika maisha yako utajihusisha na kazi nyingi sana, basi wewe zifanye. Lakini hata siku moja, usisahahu kusudi lako wewe kuwa hapa duniani. Hii ndio kazi kuu

7. Dunia ina pande mbili. UPANDE WA KILE AMBACHO KILIPASWA KUTOKEA. Na UPANDE WA KILE UNACHOPASWA KUFANYA. Sasa wewe unaiona dunia kutokea upande gani? Upande mzuri wa kuiona dunia ni upande wa kile ambacho unpaswa kufanya.

8. Tukiachana na lugha ya maneno, kuna lugha ya ambayo haitegemei maneno. Na lugha hii sio nyingine bali lugha ya upendo, kusudi la maisha na kutafuta maana ya wewe kuishi.

9. Unaposoma kitu au kuwa maarifa juu ya kitu fulani, basi usiishie tu kuyasoma, bali yaweke katika matendo. Matendo ni jambo la msingi sana kuliko kitu chochote.

10. Ukiweka nguvu yako kwenye jambo ambalo unalifanya sasa hivi utakuwa mtu mwenye furaha sana. Utaona kwamba kuna maisha kwenye kila eneo, utaona uhai kwenye jangwa, utaona nyota angani, na utafurahia sana kila kitu.

11. Unapokuwa na nafasi ya kufanya kitu siku ya leo, kifanye leo. Ni bora kujutia sasa hivi kwamba hukufanya kazi fulani miaka 10 iliyopita badala ya kuja kujutia miaka 20 ijayo ijayo kwamba hujafanya jambo ambalo ulipaswa kulifanya siku ya leo.

12. Mahusiano ya kimapenzi hayapaswi kukutenganisha wewe na kusudi lako la maisha. Kama itakuwa hivyo basi jua kwamba uhusiano huo haukuwa wa kweli.

13. Ukimpenda mtu, umpende kwa sababu ni mtu. Na kusiwepo na sababu nyingine.

14. Kuna kitu kimoja ambacho hufanya ndoto za watu kutotimilika, na kitu hiki ni uoga wa kutimiza malengo yao.

15. Kila siku ni siku yako wewe kukua kwa kujifunza. Hakikisha unakuwa tayari kujifunza kitu kipya kila iitwayo leo. Hata kama unajiona unajua kiasi gani bado hujajua tu. Jiongezee maarifa zaidi

16. Unawahitaji watu wengine kuweza kufika unapotaka.

17. Kila mtu kazaliwa kwa kusudi. Kila mtu anapotimiza kusudi lake hapo dunia inakuwa sehemu nzuri sana maana upendo unakuwa unasambazwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila mtu anakuwa anatimiza kitu fulani chenye mchango kwa mwenzake

18. Kutimiza kusudi la maisha ndio huleta upendo kwenye dunia. Mfano jua linatimiza kusudi la kuwaka na kutoa mwanga, upepo unatimiza kusudi lake la kuleta hewa safi, ardhi inatimiza kusudi lake la kufanya vitu viote. Hapo ndipo furaha  ilipo kila kitu kinapotimiza kusudi lake.

19.  Ukitaka kutimiza kusudi lako, basi unapaswa kurudi kwa muumba wako. Mtengenezaji wa kitu ndiye mwenye uwezo wa kujua kusudi la kitu.

20. Kusudi lako halitatimizwa kwa siku moja tu. Utahitaji kuweka nguvu, kujitahidi, na kuhakikisha kwamba unavumilia kuanguka kutakakojitokeza kwenye safari.

21. Unapofanikiwa kulijua kusudi lako. Ukalitimiza dunia itakulipa. Na hapo ndipo utapaswa kutoa tena zaidi kwa dunia.

Haya ni mambo 21 ambayo nimepata kujifunza kwenye kitabu cha ALCHEMIST. Ni kizuri sana kisome na wewe utapata kujifunza mambo mengi sana, sana.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blospot.com

Karibu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X