Aliyeandika Pesa Ni Chanzo Cha Maovu Yote, Hakuwa Hata Na senti Moja


Ukienda katika mazingira ya watu ambao hawana pesa, utawasikia wakisema kila aina ya ubaya juu ya pesa. Utawasikia wakisema wenye pesa hawalali, utawasikia wakisema wenye pesa hawali kama sisi ambao hawana. Utawasikikia wakijifariji kwamba hautazikwa na pesa kwenye jeneza moja…
Na mengine mengi kweli…orodha inaendelea na kuendelea.

Soma Zaidi: HII NI HAZINA ILIYOLALA KWENYE KITABU HIKI KIMOJA

Sasa waulize wana kiasi gani mfukoni? Hawana! 

Je, kupenda pesa ni chanzo cha maovu yote

Sasa baada ya hapo kutana na watu wenye pesa. Utakuta wanaongea kila aina ya mazuri ya pesa. Utakuta wanazungumzia jinsi pesa inavyosaidia watu. Wataongelea pesa inavyoleta maendeleo,
Huwezi kuwasikia wakiongea kitu hasi juu ya pesa.

Na ukiwafuatilia kweli pesa wanayo..

Sasa hapa ninapata wazo linalozunguja kwenye akili yangu. Wanaoonekana wanaisema ubaya pesa hawana pesa. Na wanaoona uzuri wa pesa ndio wenye pesa. Kumbe hata huyu jamaa aliyesema pesa ni chanzo cha maovu yote hakuwa na senti mfukoni. Yaani kiufupi iko hivyo.

Maanabpesa kama pesa sio mbaya wala sio nzuri. Pesa sio chanya wala hasi. Yaani pesa ipo katikati.

Sasa cha kufanya wewe hupaswi kuisema ubaya wowote pesa. Ipende pesa. Ndio ipende. Huwezi kupata kitu ambacho hupendi hata kidogo. Chukulia mtu anavyopata mchumba. Hakuna anayejenga mahusiano na mtu ambaye hampendi. Kama mtu humpendi basi huwezi kukaa naye. Basi hapo ndio maana nasema hivi, ipende pesa. Ndio itakuja katika njia yako. Utakaa na pesa meza moja kama unaipenda pesa. Pesa sio mbaya ubaya unaujenga wewe mwenyewe. Kama wewe unaisema ubaya pesa jua hauna😊😊😊 .
Asante sana

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X