Haribu kilichopo Ili Upate Kitu Bora Zaidi


Wahenga walisema kwamba mtaka cha uvunguni sharti ainame.  Ukifuatilia usemi huu kwa undani utagundua kwamba pale unapohitaji kitu kizuri basi kuna gharama ambayo unapaswa kuilipa kabla hujapata kitu.

Na gharama hii muda mwingine inaweza kukutaka kuharibu kitu kwanza kabla kitu kizuri hakijaonekana.

Kwa hiyo pale utakapotakiwa kuharibu kitu kwanza usishangae wala usisite kama kuharibu ndio kunaleta kitu bora zaidi.

Fundi cherehani ukimpa kitambaa, atakikata kiasi kwamba wewe hutatamani kuona vipande vinavyotokea. Ila akikiunganisha na kutengeneza nguo mwenyewe utafurahi.

 Maisha yakikutaka kuharibu kitu usisite kufanya hivyo kama kuharibu ndio kunalera ubora zaidi.

Angalia fundi seremala. Ukimpa ubao, ataukata na kutoa vipande. vipande hivyo ukiviona unaweza kufikiri fundi cherehani kaharibu kazi tayari ila ukweli ni kwamba baada ya hapo atatengeneza boonge la samani (meza, kiti, kitanda n.k).

Vitu hivi vyote kwa pamoja vinanikumbusha ule usemi wa Dale Carnegie aliousema takribani miaka 100 iliyopita. Kwamba maisha yanapokupa limau, wewe unatengeneza juisi ya limau.

Sasa hapa ni kwamba maisha yanapokulamizisha kuharibu kitu kwanza kiharibu. Ila usiishie tu kuharibu. Kijenge baada ya hapo.

Kumbuka kwamba kitu kinakuwa hakina maana baada ya kuharibiwa mpaka pale unapokuwa wewe umekiunda tena.

Sio kila nyakati zitakuhitaji kuharibu kwanza ili utengeneze tena. Hapa ndipo utapaswa kukaa chini na kufikiria
 je, hiki nacho kinapaswa kuharibiwa na kutengenezwa tena?

Je, gharama yake ya kukitengeneza ni kubwa kiasi gani?

Je, kisipoharibiwa kikabaki kilivyo kitakuwaje?

Je, kikiharibiwa madhara yatakuwaje?

Je, nikiamua kuongezea kitu kingine bila kuharibu italeta nini?

Kama utaweza kupata majibu ya maswali haya basi jua kwamba hapo ndipo unaweza kuchukua hatua ya kuharibu ili utengeneze kitu bora zaidi au usiharibu kabisa!
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Asante sana.

Soma Zaidi: Hatua Sita Za Kujenga Maisha Ya Kuigwa
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X