Hongera sana rafiki kwa siku hii ya leo. Kumbuka kwamba siku ya leo ni siku ya kipekee sana. Haijawahi kutokea wala haitakuja kutokea. Ni siku mpya, ni siku ya kipekee na siku itakayokuwezesha kufanya makubwa sana.
Leo hii tuangalie sifa moja kuu ya rafiki wa kweli. Sifa nzuri sana ya rafiki wa kweli ni kwamba atakusaidia wewe kufikia ndoto yako.
Ukiona rafiki yako anakuvuta kufanya vitu ambavyo vinakuzia wewe kufikia ndoto yako basi huna budi kuachana naye mara moja.
Moja kati ya vitu ambavyo vitakufanya wewe kufikia ndoto zako vizuri ni wewe kuweka viwango ambavyo watu unaouhusiana nao wanapaswa kuwa navyo. Moja kati ya viwango ambavyo rafiki wako wa kweli anapaswa kuwa navyo ni viwango vya kukuskuma wewe kufikia ndoto zako.
Rafiki yako kama anakuita mkanywe pombe hapo jiongeze tu.
Rafiki yako kama anakuvuta mkafanye uzinzi basi hapo angalia kwa jicho la kikubwa. Rafiki yako kama anakuvuta mkavute sigara hapo jiongeze.
Rafiki wa kweli muda wote atakusukuma wewe kufikia ndoto zako. Asante sana
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
Soma Zaidi: Lugha Moja Ambayo Ni Zaidi Ya Maneno
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA