HILI NALO NI RAHISI


Moja kati ya kauli ambayo hutumiwa na watu wa kawaida ni kauli ya jambo hili ni rahisi na mimi naliweza.

Ila mara nyingi ukiwafuatilia watu wa namna hii utagundua kwamba wao wanasema tu ili kujifurahisha.  Sio kila anayesema ni rahisi basi huwa anafanya kile kitu kuonesha urahisi wake uko wapi.

Rafiki yangu, kama unataka kupiga hatua ya kimafanikio basi usiishie tu kuongea kwamba kitu hiki ni rahisi sana. Kuwa mtu wa kutenda na kuweka kile unachoona ni rahisi katika vitendo.

Badili kile unachoona kinawezekana kwa kufanya si kwa kuongea kwamba na mimi naweza kufanya. Au kuchomekea kwamba kitu hiki ni rahisi.

Kumbuka kwamba kila mtu huwa anaona ni rahisi ila mwisho wa siku mshindi ni yule ambaye huwa anachukua hatua.
Mshindi ni yule ambaye huwa anafanya badala ya kuishia tu kusema NI RAHISI SANA.

Soma zaidi: Ni Kweli Mbwa Mzee Hafundishwi Mbinu Mpya

Habari Njema Kwa Watu Wote: Hawa Ndio Watu Unaowahitaji Ili Uweze Kuanza

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X