Zamani nilikuwa najua kwamba ili mtu aitwe shujaa, basi anapaswa kuwa ameipigania nchi yake katika vita au kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa na mtu mwingine. Yaani nilijua kwamba mpaka awe amefanya kitu kikubwa sana, sana hapo ndipo tunakuja kusema kwamba huyu ni shujaa.
Ila kumbe ushujaa sio mpaka vita. Ushujaa sio mpaka utangazwe kwenye vyombo vya habari. Ushujaa ni mfumo wako wa maisha unavyoyaishi kila siku kwa kufanya kila kitu hata kama ni kidogo katika namna ya ukubwa sana. Huu ndio ushujaa.
Hata wale unaowasikia wanaitwa mashujaa kwenye taifa letu, sio kwamba kwa siku moja tu basi waliibukia na kufanya kitu kimoja wakaitwa mashujaa.
Ukiwafuatilia utagundua kwamba NYUMA YA USHINDI WAO basi kuna kuna vitu kadha wa kadha walifanya, japo vilikuwa vinaoenekana ni vidogo kwa wakati huo ila muunganiko wa vitu hivyo ulizaa matunda makubwa sana.
Sasa leo hii nataka ufahamu jambo moja la kishujaa ambalo unapaswa kulifanya kila asubuhi. Na jambo hili sio jingine bali ni KUTOKA KITANDANI ASUBUHI NA MAPEMA WAKATI WENGINE WAMELALA. Kiukweli kwangu huu ni ushujaa mkubwa.
Huu ni ushujaa unaoweza kuupata mapema asubuhi wakati watu wote wakiwa wamelaa kabisa. Huwa napenda kuwaambia watu kwamba usingizi ni mtamu sana, ila malengo na ndoto zako ni tamu zaidi. Hivyo asubuhi unapaswa kuacha usingizi na kuelekea malengo yako na ndoto zako mara moja bila kujiuliza.
Nimekaa na watu wengi sana ambao huwa wanaweka ALARM ya kuwaamusha asubuhi. Cha ajabu huwa ikipiga huwa wanaigusa na kuiachisha ili waendelee kupiga usingizi. Narudia tena, USINGIZI NI MTAMU ILA NDOTO NA MALENGO YAKO NI TAMU ZAIDI. Hapa ndipo unapaswa kuwa makini kabisa katika kuhakikisha kwamba raha za muda mfupi hazikudanganyi kuacha kufanya mambo yako ya muda mrefu. Jijengee utaratibu maalumu kuanzia leo wa kufanya jambo hili japa la kishujaa kila siku. Yaani kuamka mapema asubuhi wakati watu wengine wote wakiwa wamelala. Ni ndani ya wakati huo huo sasa unaweza kufanya vitu ambavyo watu wengine wanashindwa kufanya.
Ni ndani ya wakati huo huo unaweza kuibua kipaji chako ambacho kimo ndani ya wewe. Ni ndani ya wakti huo unaweza kufanya kazi ambayo ni tofauti na kazi nyingine za siku yako
Kama siku yako unapaswa kuianza kishujaa basi anza na kutoka kitandani mapema sana wakati wengine wakiwa wamelala.
Soma Zaidi: Hii Ni Sentensi Iliyonichekesha Sana
KONA YA SONGAMBELE; Hili Ndilo Jambo Linalolipa Sana
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA