Jambo Moja Unalopaswa Kuliendeleza Kila Siku


Hongera sana kwa siku hii ya leo. Ni siku ya kipekee, ni siku ambayo hujawahi kukutana nayo, ni siku ambayo unapaswa kuiishi.

Ndani ya siku hii ya leo hakikisha unafanya vitu bora zaidi ya jana. Ongeza thamani zaidi ya zaidi ya jana. Kuwa mtu bora zaidi ya ulivyokuwa jana.

Usikubali leo kuiona jana kama siku iliyokuwa bora zaidi ya leo. Leo ndio unapaswa kuwa bora, bora sana. Hivyo hakikisha unaiishi vyema sana.

Soma Zaidi: Naam, Kipenga Kimepulizwa Mwaka 2018!

Ukiona mafanikio ya jana ni bora kuliko leo. Ukianza kusema kwamba afadhari jana ilikuwa bora sana. Basi hapo jua kwamba hukui. Na kama hukui maana yake unakufa. Na jambo moja unalopaswa kuliendeleza kila siku ni kukua.
Hakikisha unakua kila siku.
Sio tu ukue kiumri (maana hiyo ni asili). Lakini pia unapaswa kukua katika vipengele vingine.

Unapaswa kukua kimawazo,
Unapaswa kukua kiafya,
Unapaswa kukua kiroho
Unapaswa kukua kiuchumi
Unapaswa kukua kimahusiano.

Yaani kama kuna kitu unapaswa kukiendeleza kila siku baaasi, ni kukua kila siku.

Je, leo utakua katika nini leo.

Andika vitu vitatu unavyoenda kuvufanyia kazi leo hii.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X