Kama Huoni Thamani Ya Kitu Hiki Basi Huwezi Kuona Thamani Ya Vitu Hivi.


Kuna vitu huwa hatuoni thamani yake katika udogo wake, tukisubiri kuja kuona thamani ya vitu hivyo vitakapokuwa  vikubwa sana.

Ila ukweli ni kwamba  kama hujaona thamani ya vitu vidogo basi huwezi kuona thamani ya vitu vikubwa.

Kama huoni thamani ya shilingi mia moja basi hutaona thamani ya laki.

Kama huoni thamani ya dakika moja basi huwezi kuona thamani ya saa.

Na kama huoni thamani ya saa moja basi hujajua thamani ya maisha.

Kama huoni thamani ya mtu mmoja huwezi kuona thamani ya watu kumi.

Na kama huoni thamani ya watu basi ni vigumu  kwako kununua muda wa watu

Kama hununui muda watu basi hujajua kwamba muda una kikomo

Kama hujajua kwamba muda una kikomo basi utafanya kazi muda mwingi lakini utachelewa kufikia mafanikio makubwa maana uko peke yako

Kama huoni thamani ya kidogo hutajua thamani ya kikubwa.

Anza leo hii kuona thamani ya kila kitu kinachokuja mbele yako. Ione thamani ya dakika moja, ione thamani ya saa. Ione thamani ya wiki ione thamani ya mwaka

Ione thamani ya shilingi mia, elfu, laki ndipo utafurahia na thamani ya milioni.

Soma Zaidi: TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-118, tatizo unakamuliwa na muda
UMUHIMU WA DAKIKA MOJA
Hili Ni Jambo Linalofanya Watu Washindwe Maishani

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X