Habari ya siku hii njema sana ya leo. Hongera sana kwa aiku hii ya kipekee sana. Kwa hakika hii ni siku ambayo unapaswa kuitumia vyema sana.
Siku zinazidi kukimbia kila kukicha. Na kila siku inayopita basi hiyo hairudi. Wakati huu unabaki kuwa wakati pekee wa wewe kupangilia ratiba zako na kufanya mambo makubwa.
Kama leo hii utahairisha kitu na kuacha kukifanya leo. Mwaka mmoja kutoka sasa utakuwa unalia kwa sababu ya hivi vitu ambavyo hujafanya leo. Sasa badala ya wewe kuja kulia siku moja kwa sababu hukutumia muda utumie sasa. Kama umepanga kufanya leo kifanye.
Kamwe usihairishe kitu unachoweza kukifanya leo kwa kisingizio cha kuja kukifanya kesho.
Siku zote muda mzuri wa kufanya kitu ni leo. Kumbuka kuna usemi wa ukweli na wa uhakika ni kwamba leo ni leo, asemaye kesho ni mwongo.
Asante sana, tukutane kwenye jukwaa letu la wanamafanikio.
Soma Zaidi: TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-121
tatizo hujanoa shoka lako
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA