Kosa Moja (01) Yanayofanywa Na Watu Wakati Wa Usomaji Wa Vitabu


“Ukitaja kumficha mwafrika kitu basi kiandike katika kitabu” ni usemi wa Kiafrika. Usemi huu unaashiria kwamba waafrika sio wasomaji wa vitabu.

Tafiti zinaoenesha watu “wengi sana huwa wanakufa katika umri wa miaka 20 na kusubiri kuzikwa wakiwa na umri wa miaka 80″. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wanapofikia umri wa miaka 20 wengi ndipo wanatoka kwenye vyuo na kuhitimu maeneo mbali mbali. Hata hivyo baada ya kuhitimu watu wengi sana huwa wanaona kwamba ndio wamemaliza kila kitu. Hivyo kwao  kusoma sio tena kitu cha maana. Hivyo hakuna hata mtu mmoja ambaye huwa anahangaika kuhakikisha anapata maarifa mapya.
Na kwasababu sasa hivi maarifa yanabadilika kila siku, basi hawa watu wasiopenda kujifunza hupotea kabisa.

Mbali na kwamba watu hawapendi kujifunza haswa kwa kusoma vitabu, ila wapo wachache sana wanaosoma vitabu. Na hawa wachache wanaosoma vitabu kuna kosa moja ambalo huwa wanafanya. Kosa hiki sio jingine bali kusoma kitabu nusu.

Ni mara nyingi sana watu huanza kitabu kukisoma kitabu na kinapofika nusu mtu anahisi tayari anajua kila kitu hivyo hawezi kuendelea na usomaji wa kitabu.

Kitabu kizuri ni kile utakachosoma mpaka mwisho. Kumbuka kwamba sio vitabu vyote utasoma kila kitu maana kwa kutumia usemi wa Bacon kwamba “baadhi ya vitabu vinapaswa kuonjwa, vingine vinapaswa kutafunwa, vingine vinapaswa kumezwa, vingine kumezwa na kumeng’enywa”.
Sasa rafiki yangu, kama utaamua kusoma kitabu kwa kukimeza na kukimeng’enya basi fanya hivyo. Unapaswa kuwa na vitabu vya namna hii ambavyo utasoma hadi kymeng’enywa. Na hivi ndivyo nakutaka wewe leo hii usiwe unavisoma nusu. Nataka uwe unavisoma mpaka mwisho. Yaani uvisome bila kuacha kitu.

Nimegundua kadri unavtokuwa unasoma vitabu nusu nusu, kuna maarifa mengi sana unakuwa unayaacha. Maarifa muhimu sana.

Rafiki yangu penda kusoma na soma vitabu mpaka mwisho, hakika utafurahi sana.
Soma Zaidi: Hii Ndio Sifa Ambayo Kila Kiongozi Anayo

Hivi Ndivyo Unaweza Kusoma Kitabu Kwa Wiki Moja (Mbinu Nne Za Uhakika)

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X