Maeneo Manne (04) Ya Kupata Vitabu Mtandaoni Bure


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya kipekee.

Moja kati ya vitu ambavyo nasisitiza kila siku ni kusoma vitabu.  Kusoma ni njia rahisi ta kupata maarifa ya ambayo watu wameyafanyia utafiti na wewe unakuwa una uwezo wa kuyapata yale maarifa ndani ya siku, wiki au mwezi kulingana na spidi yako ya usomaji. Maarifa haya watu wanaweza kuwa wametumia zaidi ya miaka 30 kuyatafuta na kuyafanyia majaribio, lakini wewe unayapata ndani ya masaa au siku kidogo sana.

Leo hii napenda kukutajia maeneo manne (04) muhimu unayoweza kupata vitabu vya kusoma katika kila siku ya maisha yako.

1. LIBRARY GENESIS
Huu ni mtandao wenye aina mbali mbali ya vitabu. Ukiingia humu unaweza kuandika jina la kitabu au jina la mwandishi na vitabu vyake vitaoneshwa. Utachagua kitabu ukipendacho na kukisoma
Bonyeza hapa kupata vitabu hivi

http://gen.Lib.rus.ec

2. ALIVE ONLINE LIBRARY
Hii ni maktaba ya mtandaoni ambayo inaendeshwa na mtanzania mwenzetu. Ni maktaba nzuri sana yenye kila aina ya kitabu. Unaweza kuitembelea kwa kubonyeza hapa

 https://t.me/AliveGroupThinkDifferent

3.  CHRISTIAN e-LIBRARY
Hii ni maktaba ya kikristu ambayo inatoa vitabu vya kila aina haswa vya kikristu. Katika maktaba hii unaweza kuomba kitabu au kutuma kitabu tu. Na sio vinginevyo.
Unaweza kuitembelea maktaba hii kwa kubonyeza hapa

https://t.me/joinchat/D864SUMF02Y8YnURHC1_OQ

Soma Zaidi; Makala maalum kwa Watu Maalum: Kwa Nini Kusoma Vitabu?

4. GOOGLE
Unaweza pia kuingia google ili kupata vitabu. Ukiingia google basi andika jina la kitabu na mwandishi au jina la kitabu tu, mwisho malizia na neno pdf. Kama kitabu unachotafuta kinapatikana bure utakipata.
Mfano unaweza kuandika  MADE IN AMERICA BY SAM WALTON PDF.
Kwa kuandika hivi google itakuletea machaguo mbali mbali. Mara nyingi huwa nachagua chagua la kwanza au la pili.

Kwa kutumia njia hii, chaguo zuri ni lile ambalo ukibonyeza hapo hapo linaanza kupakua wala sio kufunguka ili kuleta maneno au matangazo.

Asante sana hizi ndizo sehemu unazoweza kupata vitabu bila kulipa hata senti. Wiki ijayo nitaelekeza njia ya kupata vitabu vilivyosomwa bila kulipa senti hata moja.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


One response to “Maeneo Manne (04) Ya Kupata Vitabu Mtandaoni Bure”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X