Neno Hili Litakufanya Upendwe Na Watu, Na Neno Hili Litakufanya Uchukiwe Na Watu


Habari rafiki. Hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Leo ni siku njema sana kuwahi kutokea duniani.

Miongoni mwa njia za mawasiliano anazotumia binadamu ni maneno. Kwa siku mwanaume anasemekana anatamka maneno 7,000 huku mwanamke akitamka maneno 20,000.

Kati ya maneno hayo yote yanayosemwa kwa siku moja, kuna maneno mawili muhimu sana ambayo yakitamkwa yatakufanya upendwe au uchukiwe na watu.

Moja kati ya neno litakalokufanya upendwe ni NDIO.
Watu wanapenda sana kusikia ndio zako nyingi nyingi. Watu wanapenda wakikuambia kitu fulani kinaenda hivi wewe uitikie NDIO. Watu wanapenda wakikwambia tukafanye kitu fulani wewe uitikie mara moja NDIO.
Wakikuambia tukopeshe pesa zako wewe uitikie mara moja NDIO.

Ndio yako watu wanaipenda sana ila unapaswa kuwa mgumu kuitoa. Ni vitu vichache sana vinahitaji NDIO yako. Naam, ni vichache mno. Kwa hiyo badala ya kusema ndio muda mwingi utapaswa kusema HAPANA.

Neno hapana litakupunguzia umaarufu.
Nikiwa mdogo, nilikiwa naachiwa nyumba yetu yenye kila rasilimali ndani yake. Sasa watu walikuwa wanataka niwape vitu mbali mbali. Nilikuwa nasema HAPANA. Umaarufu wangu ulipotea. Watu wakaanza kujenga uhasama na mimi bila sababu za msingi.

Lakini kadri nilivyokuwa nasema hapana ndivyo nilikuwa nalinda rasilimali nyingi sana.

Watu hawapendi kuisikia HAPANA yako  ila wewe unapaswa kuwa mtu wa kulitumia neno hiki kadri uwezavyo.
Hapana yako ni muhimu sana kuliko ndio yako.
Kuna watu wanakubali kitu kwa nje huku wakijua kabisa kwamba ndani yao hawajakubali ila wanasema tu NDIO.
Kuna watu wamejikuta wameingia kwenye mikataba mibaya kwa sababu ya kusema NDIO kwa kila kitu..
Kuna watu wamejikuta kwenye mahusiano mabaya kwa sababu ya kupenda kusema NDIO badala ya kusema hapana.

Asante sana rafiki yangu,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X