NIKIWA MKUBWA


Kila mtoto huwa na ndoto fulani katika maisha yake.
Ukiwasikiliza watoto wadogo utasikia wakisema maneno kama,
Nikiwa mkubwa nitakuwa raisi wa nchi hii
Nikikua nitakuwa daktari
Nikikua nitakuwa kama fulani….

Na wewe unayesoma hapa kuna siku ulikuwa mtoto. Kuna ndoto ulikuwa nazo si ndio?
Je, ulikuwa na ndoto zipi? Ulitaka kuwa nani?

Sasa leo hii napenda nikuulize? Ziko wapi hizo ndoto zako za utotoni ulizokuwa nazo?
Je, umeziweka wapi? Je, unafanya nini sasa hivi? Je, unachofanya kinaendana na ndoto zako za utotoni.

Utafiti unaonesha kwamba ni asilimia 6 peke yake huwa inafikia ndoto za utotoni, hii ina maana kwamba asilimia 94 wote huwa hawafikii ndoto hizi nzuri za utotoni.

Kwa hiyo wale madaktari, walimu, wanasheria, madreva, marubani woote wa utotoni huwa wanaenda kufanya kitu kingine tofauti na ndoto za utoto wao???

Sasa swali la kujiuliza kunatokea nini hapa kati kati?
Kwa nini wengine huwa hawawezi kufikia ndoto zao?
Maisha ni mazuri sana kiasi kwamba unapaswa kuyafurahia kila wakati. Maisha hayatoi unachotaka pale unapokihitaji. Kwa hiyo wewe kusema tu napenda kuwa mtu fulani haitoshi. Na ukishasema hivyo utakutana na vikwazo, utavutwa huku na kule.
Kama kila mtu angepata kile anataka pale anapokitaja kutoka kinywani mwake basi hata asingeona thamani ya hicho kitu.

Kwa hiyo maisha yametuacha tuwe vinganganizi mpaka pale tutakapopata kile tunahitaji.  Watoto wadogo  wanapokuwa na ndoto zao wanakuwa bado hawakutana na kashi kashi za hapa na pale. Lakini zinapojitokeza hapo ndipo wengi huanza wengi huacha na kuzisahau ndoto zao.

Je, wewe unakumbuka kitu gani kilikufanya uzisahau ndoto zako?
Je, wewe kitu gani kimekukwamisha mpaka hapo?

Kama ndoto hizi umeziacha sasa hivi kinachofuata ni wewe kuhakikisha hauchi kile ambacho unakigusa. Kila wakati hakikisha kila unachopanga unakifikisha mwisho.

Haujalishi unakutana na vikwazo kiasi gani Unapaswa kuwa king’ang’anizi mpaka kieleweke


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X