Kila mtu kazaliwa na kipaji ndani yake. Yaani mtu anapozaliwa anakuwa na vipaji kati ya 500 mpaka 700. Ila kadri mtu anavyokua kulingana na mazingira, elimu, maarifa, n.k kuna baadhi ya vipaji vinaachwa pembeni na kile kitu ambacho mtu anaweka nguvu yake zaidi ndicho ambacho mwisho wa siku kinaibuka na kukua zaidi.
Kipaji ni kitu cha asili. Yaani tunacho tu ndani yetu. Haihitajiki gharama yotote ile kununua kipaji. Ndio maana mwandishi John C. Maxwell anasema “ Kipaji ni bei rahisi sana kuliko chumvi”.
Hauhitaji hata senti moja kununua kipaji. Hauhitaji mtaji wa kununua kipaji.
Hauhitaji mkopo ili upate kipaji. Kipo yaani kipaji ni bei chee sana.
Sasa kutokana na usemi huu nimeanza kuona kwa nini watu wengi sana huwa wanachezea vipaji vyao na hawavitumii.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wanapenda na wanathamini sana vitu walivyogharamikia. Ndio maana utakuta mtu anatunza vizuri sana chumvi yake kwenye kopo safi kabisa lilioshwa. Kwa nini, kwa sababu amenunua chumvi…
Lakini ulizia kipaji ambacho kinapatikana bure ulizia kipo wapi? Kimezikwa hata hakijulikani kipo wapi?
Hapa ndipo utajua kwamba vya bure havithaminiwi. Kumbe chumvi japo inanunuliwa gharama kidogo inathaminiwa zaidi ya kipaji.
Kumbe kuwa na kipaji tu haitoshi. Unahitaji kuanza kukithamini.
Pili kulipa gharama ya kukuza kipaji chako ni muhimu sana. Na juhudi unayoiweka kuhakikisha kipaji chako kinakung’arisha.
Rafiki yangu kuwa na kipaji peke yake haitoshi. Ila juhudi yako katika kukuza kipaji chako ni muhimu sana.
Ukiona mtu anang’aa na kipaji chake, usianze kusema kwamba huyu jamaa ana bahati, au huyu jamaa aligusa tu mambo yakaiva. Unapaswa kujua kwamba NYUMA YA USHINDI WA KIPAJI HIKI KUNA JUHUDI, KAZI, KUJITUMA n.k
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA