UCHAMBUZI WA KITABU SCREW IT, LETS DO IT


Mwandishi: Richard Branson
Mchambuzi: Godius Rweyongeza

Richard Branson ni mjasiliamali na mwanzilishi wa kampuni ya Virgin. Ni moja kati ya watu wacuache sana ambao wanachukua hatua za hatari. Katika kitabu chake SCREW IT, LETS DO IT ametushirikisha mambo mengi sana. Haya hapa ni mambo 17 kutoka kwenye kitabu chake.

1. Kuanza kazi ndio sehemu muhimu sana kwenye kazi.  Kwa hiyo kama kuna kitu ambacho unataka kufanya wewe anza tu.

2. Huhitaji cheti cha chuo chochote ili uruhusiwe kuanza.  Kikubwa ni wewe kujua unafanya nini na kuanza. Kwa hiyo kama ungependa kuandika, anza hakihitajiki cheti. Kama unaamua kufanya biashara, anza hakihitajiki cheti. Ndio hivyo tu.

3. Kama kuna kitu ambacho unapaswa kukifanya sasa hivi na hujakifanya basi jua kwamba hutakuja kukifanya. Hivyo tu.

4. Ukitaka kufanya kitu kizuri kwenye maisha unapaswa kujiandaa kwa kuweka mpango na kuufanyia kazi mara moja.

5. Watu wengi huulizia siri ya mafanikio kwenye maisha. Ila mafanikio kwenye maisha na biashara hayana kanuni. Ila kitu kimoja ni muhimu sana. Fanya kazi kwa bidii, amini inawezekana na furahia kazi yako.

6. Kupata pesa halipaswi kuwa lengo la maisha yako. Kwa sababu pesa ni matokeo ya thamani na kazi ambayo umeifanya. Tafuta kazi ya kufanya, ifanye kwa bidii na hakikisha kazi hiyo inatatua matatizo ya watu.

7. Mambo yanapoonekana kutoenda vizuri kama inavyotegemewa usiache kufurahia.

8.  Usisubiri mpaka kusataafu ndipo uje kufurahi, kula vizuri na kufanya mazuri. Maisha yako ya kila siku yanapaswa kuwa katika mtindo huu.

9. Kama una wazo la kibiashara, usiogope kulianza katika udogo wake.

10. Kama unapaswa kufanya kazi ambayo huipendi, sasa usiendelee kulia. Badili mtazamo wako. Anza kufanya kazi kwa bidii, ipende kazi na ifurahie. Ona chanya kila wakati kwenye kazi yako. Kama bado hufurahii kazi, basi weka lengo la kuachana nayo.

11. pale utakapoamua kuchukua hatua kubwa kwenye maisha kuna watu watakukatisha tamaa kulingana na ukubwa wa hatua utakayochukua. Hapo ndipo utahitaji kuwa wewe na kufanya maamuzi magumu.

12. Ukisema kwamba utafanya kitu fulani hakikisha unakifanya. Usiwe mtu wa kubadili maneno yako mara kwa mara. Yaani kwamba zamu hii unaamua nitafanya hiki bila kufanya baadae unasema kingine. Kiufupi ni kwamba hakikisha neno lako unalolitamka linakuwa kama sheria.

13. Kuna wakati utashinda na kuna wakati hutafanya vizuri kabisa. Sio kwamba kila maamuzi yako yatakuwa sahihi kwa asilimia 100 kila siku. Furahia pale unapofanya maamuzi bora na kufanikiwa. Usilie wala kulalamika pale ambapo utafanya maamuzi mabovu au kukosea.

14.  Siku  zote weka malengo makubwa sana maishani mwako.

15. Usiridhike na kile uluchonacho. Kila wakati nenda hatua za ziada zaidi ya hapo ulipo. Nenda hatua ya ziada kila wakati.

16. Vitu unavyovipata kwa nguvu zako wewe mwenyewe unavithamini sana kuliko vitu ambavyo unapewa bure.

17. Muda mzuri wa wewe kuishi ni sasa hivi. Kwa hiyo hakikisha unaitumia sasa hivi kuliko unavyoutumia muda mwingine.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X