Unapaswa kuwa na ndoto kubwa sana za maisha ambazo unazifanyia kazi. Usiishi tu ilimradi unaishi. Usifanye tu ilimradi unafanya. Bali hakikisha unafanya kweli kazi ukiwa unajua unaelekea wapi. Na sehemu nzuri unapoweza kuelekea ni kwenye ndoto yako kuu ya maisha.
Je, unayo ndoto?
Je, unataka kufikia nini baada ya miaka mitatu mpaka mitano?
Unataka kuwa unamiliki nini baada ya miaka kumi kutoka sasa hivi?
Je, miaka thelathini kutoka leo unajionaje?
Ndoto yako hata kama itakuwa kuvwa sana kiasi gani hakikisha unaifanyia kazi kila siku bila kuacha. Anza kufanya kile unachoweza kufanya leo. Endelea kufanya kile kinachoonekana hakiwezekani. Mwisho wa siku utajikuta unaweza hata kile ambacho hakiwezekani.
Soma zaidi: ANZA KUTUMIA KILE ULICHONACHO
Hivi Ndivyo Watu Wanaweza Kufikia Malengo Makubwa Sana
Asante sana.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA