Vikwazo Viwili (02) Vikubwa Cha Ukuaji


Habari ya siku hii njema sana rafiki.
Mara nyingi mtu akiwa anaanza kitu huwa anaanza kwa motisha kubwa sana. Utakuta mtu anakuwa na moto wa kufanya kitu kiasi kwamba humwambii kitu.

Utasikia mtu anakuambia yaani fursa fulani inalipa sana na mimi ngoja niifanye. Hapo mtu anakuwa anajua mazuri mengi ya jambo husika.

Kadri siku zinavyozidi kusogea motisha ile inazidi kupotea. Sasa hapo unadhani ile motisha huwa inapotelea wapi? Hapa kuna maadui wawili wanaowakumba watu wengi.

1. Mafanikio madogo
Mafanikio madogo yanaweza kuwa ni adui wa mafanikio makubwa. Yanakufanya ujione umefika kumbe bado. Yanakufanya ujione wewe ni bingwa wakati bado una safari ndefu sana.
Rafiki yangu,usitulie na mafanikio madogo bali kila wakati kazana kupata zaidi. Kuwa na kiu ya kitu kikubwa zaidi. Kuwa na kiu ya kusonga mbele kila wakati.

2. Kuridhika
“kuridhika ni adui wa mafanikio”
Kuridhika kunatokana na utulivu. Vitu vilivyotulia havina historia nzuri. Mbu waliotulia  husababisha malaria.
Konokono waliotulia kwenye maji huleta magongwa.
Kwa hiyo kutulia sio kuzuri. Kila mara penda kwenda hatua ya ziada. Kamwe, kamwe, kamwe usitulie na kidogo.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X