WHEN ONE PLUS ONE DOES NOT BECOME TWO: Mambo Matano Ya Kufanya Ndoto, Malengo Na Maono Yako Yanapoenda Kinyume Na Matarajio


Kwa kawaida moja na moja ni mbili,
njiti ikigusishwa na kiberiti moto huwaka na chumvi ikiwekwa kwenye maji itayeyuka.

Hayo yote niliyotaja hapo juu yanatokea kwenye hali ya kawaida.

 Ila kuna nyakati moja na moja huwa haziwi mbili. Kuna nyakati njiti ikigusishwa na kiberiti, moto hauwaki. Na kuna nyakati chumvi kwenye maji haisagiki.

Je, nataka kusema nini hapa?
Ninataka ujue kwamba wewe ni mshindi na kuna malengo ambayo umeyaweka, ambayo unapaswa kuyatimiza.

Lakini sio kila wakati malengo yako, ndoto zako na maono yako yataenda kama unavyotegemea. Hapo ndipo utajihataji kuweka nguvu ya ziada. Hapo ndipo utahitaji kufikiri nje ya kumi na nane ili uweze kusonga mbele hata kama unaona mambo hayakaa vyema.

Hapa napata nguvu kusema kwamba John C. Maxwell aliposema kwamba kipaji cha mtu peke yake hakitoshi. Alikuwa tayari  anajua kwamba sio muda wote moja kujumlisha moja huleta mbili. Ndio maana unahitaji nguvu ya ziada.

Sasa hapa nimekuandalia mambo matano ambayo unapaswa kuyafanya pale  malengo, ndoto na maono yako yanapoenda kinyume na matarajio yako.

1. JIULIZE GHARAMA AMBAYO HUJALIPA.
Kuna usemi mmoja wa Kiafrika unaosema kwamba “ukitaka kwenda kasi kimbia peke yako, ila ukitaka kufika mbali tembea na watu”. Sasa usemi huu kwa leo naomba tuubadilishe na tuuweke hivi, “ukitaka kufanikiwa haraka pitia njia ya mkato, ila ukitaka mafanikio ya kudumu kubali kulipa gharama”
Sasa rafiki yangu kuwa tayari kulipa gharama kila siku. Lipa gharama ya kile unachohitaji. Ukiona kuna kitu kwenye maisha yako hakiendi vizuri basi hapo ni muda wa wewe kukaa na kujiuliza, ni wapi hapo ambapo wewe hukulipa gharama?
Kumbuka gharama ya kitu sio lazima iwe pesa, inaweza kuwa ni muda, inaweza pia kuwa ni nguvu n.k

Kaa leo ujiulize ni wapi hapa ambapo sijalipa gharama?

2. USIMLALAMIKIE MTU
Kama unaona kitu hakiendi kama unavyotarajia, usikimbilie kutafuta mchawi wa kitu hicho hapo. Nina hakika ukimtafuta mchawi huwezi kumkosa. Mchawi yupo tu, ila ukifuatilia utagundua mchawi mkubwa ni wewe.

Najua utalalamika kwamba kama asingekuwa fulani, basi hiki kisingekuwa hivi. Au kama si huyu basi kisingeenda vile. Lakini unapoteza muda. Hiyo ilikuwa ni jana. Sasa hapa ni muda wako wewe kufanya mabadiliko makubwa sana. Ni muda wa wewe kuweka nguvu kwenye leo badala ya kuillamikia jana.

3. PANGA MBINU MPYA ZINAZOFANYA KAZI.
Kuna mbinu, umetumia jana ila hazijafanya kazi ndio maana hujaweza kufika ulipotaka.

Tatizo sio kile unachofanya. Tatizo ni jinsi unavyokifanya. Hivyo kama mbinu fulani haifanyi kazi, basi fanya kwa namna nyingine ili mambo yaende kama inavyotakiwa.

4. JIULIZE SOMO ULILOPATA KUTOKA KWENYE HICHO KITU
Kila kosa huja na mbegu ya ushindi. Aliandika Npolleon Hill miaka kadhaa iliyopita.
Kwa hiyo kushindwa kwako kutimiza lengo fulani lazima kumekuja na kitu fulani ambacho ulikuwa hujui. Sasa kaa chini ujiulize hiki ni kitu gani. Ukikaa vizuri kitu hiki utakipata tu.

5. JIULIZE NI ELIMU GANI UNAKOSA
Moja kati ya usemi maarufu kutoka kwenye Biblia ni usemi wa pasipokuwa na maarifa, watu huangamia.

Na wewe inawezekana chanzo cha wewe kutofanikisha mambo yako kikawa ni elimu kidogo ambayo unayo kuhusu hicho kitu.
Sasa ni muda wa wewe kuweka juhudi zaidi kutafuta maarifa ili hicho kitu ulichoshindwa uweze kukifanya kwa ubora zaidi siku nyingine.

Hayo ni mambo matano ambayo unapaswa kuyafanya, pale mambo yanapoenda kwenda kinyume na matarajio yako.

Asante sana.
Ndimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391

💥jana nimezindua kitabu cha JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO.
Kitabu hiki ni soft copy na kinapatikana kwa sh. 4,000/ kwa siku tano tu kuanzia jana.

💥chukua hatua ukipate kitabu hiki kabla hakijarudi kwenye bei yake ya kawaida.

💥lipia sh. 4,000/- kwenda 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA.

💥baada ya hapo nitumie email yako. Utapokea kitabu, punde tu baada ya kutuma email yako.

Karibuni sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X