Kitu Hiki Kitafanya kila Mtu Apende Kukusaidia


Najua kwamba kila mtu angependa watu maarufu, viongozi wakubwa, wanampira wenye majina, wanamziki na waigizaji nguri wawe marafiki zake.

Kila mtu angependa awe nao na kupiga nao picha (selfie) muda wowote ambao yeye atajisikia.

Najua wengi wangependa kukutana na DIAMOND PLATNUMZ ili kupiga naye stori. Najua wengine wangependa kukutana na raisi Magufuli.

Hata kama hawataongea naye, ila ile hali ya kukutana na mtu mkubwa kama Magufuli watu wanaipenda sana. Yaani inaweza kumpaisha mtu na kumfanya maarufu ndani ya muda mfupi sana.

Ila watu wa namna hii ni vigumu sana kukutana nao. Ni vigumu mno wako bize kiasi kwamba hawezi kukaa na kufikiri kwamba kuna mtu kama wewe.  Maana watu hawa nakuhakikishia kwamba wapo bize sio utani.

SOMA ZAIDI: TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM.

Ila binafsi nimegundua njia rahisi ya kukutana na watu hawa. Yaani kwa njia hii utakutana na mtu maarufu ambaye unampenda bila kipingamizi.

Ni njia rahisi sana kiasi kwamba nashangaa kwa nini sikuwahi kuijua njia hii kabla. Nashangaa sana. Nashangaa pia kwa nini watu walio wengi hawajahi kuijua.  Ila kwa sababu mimi Godius Rweyongeza nimeijua, basi naona nikushirikishe na wewe itakufaa sana.

Njia yenyewe ni kutaka kuwasaidia watu hawa.

 Kama  kuna mtu maarufu ambaye unataka kukutana naye. Basi angalia namna ya wewe kumsaidia kwanza na mwisho wa siku wewe atakusaidia na wewe utanufaika zaidi.

Hali hii inaitwa win win principle. Yaani wewe unafaidika na yeye anafaidika.

Ngoja nikwambie kisa cha rafiki yangu ambaye aliwahi kuja kwangu siku si nyingi.

Rafiki yangu, ana ndoto ya kuwa muigizaji maarufu sana. Ila yeye anachotaka ni kuigiza na waigizaji maarufu akina VICENT KIGOS, JB na wengine.

Swali langu kwake lilikuwa umefanya nini ili upate nafasi ya kuigiza na watu hawa?

Alinijibu hivi, nimejaribu kila njia ila nimeshindwa.

  Nimetumia nafasi hiyo kumwambia hivi rafiki yangu:
Moja, andika waigizaji kumi ambao unapenda kuigiza nao..

Pili, tafuta njia ya kuwasaidia watu hawa. Unaweza kuandika maigizo mazuri sana kiasi kwamba wakiyaona watapenda kuyaigiza. Na ukampatia kila mmoja la kwake mwisho wa siku utajikuta na wewe wanakuita ukaigize nao. Kwa jinsi hiyo utakuwa umepata nafasi ya kuonesha kipaji chako zaidi na zaidi.

Rafiki yangu na wewe popote pale ulipo, basi itumie njia hii.

Asante sana, tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X