Mambo Saba Ya Kujifunza Kutoka Kwa Simoni Petro


Petro alivua samaki usiku kucha bila kupata hata samaki mmoja. Hakupata hata mmoja!!!

Ilipofika asubuhi alikuwa amechoka sana, na amekata tamaa.

Lakini Yesu alimwambia endesha mashua mpaka kilindini mkatupe nyavu zenu, mpate kubua samaki (Luka 5:4).  Petro alipofanya hivyo alipata samaki wengi sana. Kiasi kwamba walijaza mashua yao na kuanza kuwapungia mkono wenzao ili waje kuwasaidia.

Soma Zaidi: Mafunzo Matatu Kutoka Kwa Viwavi

SOMO:
1. Inawezekana umekuwa unazunguka hapo hapo kila kwa siku nyingi sana.  Na umefikia hatua ya wewe kukata tamaa. unataka kuacha na kwenda kujaribu mahali pengine.

Naomba nikwambie kitu. Usiondoke ebu tweka mpaka kilindini.

Sawa akina Petro walikuwa wanavua usiku kucha, ila uvuaji wao ulikuwa namna gani. Inawezekana walikuwa wanazunguka hapo beach usiku mzima na hawakupata samaki.
 Mwenye maarifa zaidi yao basi akawaambia, “HAPANA ebu peleka  nyavu zenu mpaka kwenye maji marefu sana.”

Waliweza kupata samaki wengi sana.

2. Kitu cha pili cha kujifunza ni kwamba usifanye vitu kwa mazoea. Petro alikuwa mvuvi wa siku nyingi sana. Lakini alikuwa  anavua kwa mazoea. Laiti asingeambiwa peleka nyavu zako hadi kwenye maji marefu angeendelea kuvua kwa mazoea.

3. Tatu tunapaaswa kuwa tunawatafuta watu wenye uelewa zaidi yetu ili tupate ushauri kutoka kwao. Hawa ni watu ambao wamefanya kile ambacho tumefanya na wamekifanikisha, au watu wenye uelewa na ujuzi zaidi kwenye sekta hiyo. Achana na ile imani ya nitafanya mimi bila msaada.

4. Nne tunapata mwanga kwamba maarifa ni bora zaidi kuliko nguvu. Akina Petro walikuwa sijui kwenye zama gani. Yaani walikuwa wanakimbizana na manguvu yao ili wavue bila maarifa.
Akaja Yesu, na maarifa yote juu ya elimu ya bahari. Pale pale alipowaambia wakavue ndipo walipata samaki wengi sana kiasi cha kujaza mtumbwi.

Ebu na wewe anza kutafuta maarifa. Ndio anza kutafuta maarifa zaidi  ulimwengu wa sasa hivi unaendeshwa na maarifa zaidi ya unavyoendeshwa na nguvu.

Jeshi kubwa sana lenye mamilioni ya watu, linaweza kupigwa na kajamaa kamoja knakofiki sana na kutumia maarifa.

SOMA ZAIDI: Uchambuzi wa kitabu, SCREW IT, LETS DO IT
5 . Tano, vitendo vinalipa zaidi ya maneno.
Nipo najaribu kufikiri kama Petro angembiwa peleka nyavu kule akaendelea kupiga soga pale ingekuwaje.

Maana Petro alikuwa mwenyeji pale na bila shaka watu wengi sana walikuwa wanamfahamu.
Sio hilo tu, siku hiyo kulikuwa na watu wengi sana. Maana ile anaambiwa apeleke nyavu kwenye maji marefu ndipo walikuwa wametoka kumsikikiza Yesu.  Na Biblia insema “… watuwengi walikuwa wamemzunguka [Yesu] wakisongamana”.

Hii ndio kusema pale mwaloni walikuwepo watu zaidi ya ile idadi ya kawaida iliyozoeleka.

Kwa hiyo kwa Petro huo ulikuwa muda mzuri wa kujamiiana au kusocialize na kufahamiana na watu. Na pengine kujuliana hali.
Ila Petro aliamua kuweka kazi na kuachana na maneno.

6. Sita, Tunajifunza kwamba Utii ni bora sana kuliko kiburi.
Ona hapa, “…Baada ya Yesu kuingia kwenye Mashua Moja ikiyokuwa ya Simoni, alimtaka simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa maji”.

Yaani hapa nashangaa,
Simoni ni mvuvi. Yesu anahubiri. Hawa watu hawajahi kukutana hata siku moja. Ila Huyu Yesu anakuja anakaa kwenye mashua ya Simoni. Sasa kwa nini Simoni hamkatazi Yesu kuingia kwenye mashua yake?

Katika hali ya kawainda vijana tunasema kingenuka. Yaani, hali ya hewa ingebadikika maana, Yesu alipanda tu mashua ya watu. Ila Simoni alikaa kimya.

Na bado alitii na alipoambiwa asogeze mashua kwenye maji  mbali kidogo na  watu.

Petro anatii. Yaani ananishangaza sana.
Kwanza hamjui Yesu,.
Halafu anasogeza mtumbwi,
Na bado anakaa kusikiliza.

Hapa tujifunze kwamba utii ni bora sana kuliko kiburi.

7. Saba, ukiona umeelemewa usikose kuwashirikisha watu wakusaidie. Ona alichofanya Simoni, aliwaita wenzao waliokuwa katika mashua nyingine, ili waje kusaidia.

TUKUTANE KWENYE JUKWAA LETU LILEE LA WANAMAFANIKIO,

SOMA ZAIDI: Sababu Nne (04) Zitakazokufanya Ukumbatie Matatizo

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X