Usikose Kufanya Jambo Hili Kila Iitwayo Leo


Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii ya leo. Leo hii ni siku bora sana kuwahi kutokea kwenye dunia hii. Rafiki yangu naomba uitumie vyema sana siku hii ya leo.

Kitabu hiki kipo kwa ajili yako
Tuwasiliane 0755848391

Kila iitwayo leo kuna kitu kimoja ambacho hata kama inakuwaje hupaswi kuacha kukifanya.
Kitu hiki kitakufanya ukue kiakili, kiafya na kipesa. Kitu hiki kitakufanya tajiri kiroho, kimwili, kiakili, kipesa, kiafya, na kimahusiano.

Soma Zaidi: Faida Moja Ya Kujifunza Ambayo Hujawahi Kuambiwa Popote

Kitu hiki sio kingine rafiki yangu bali ni kujifunza.
Kujifunza kuna uwezo wa kubadili kilaza kuwa gwiji
Kujifunza kuna uwezo wa kumfanya mwanafunzi kuwa mwalimu
Kujifunza kunaweza kukufanya uamushe ubunifu ulio ndani yako
Kujifunza kutakufanya uione dunia kwa jicho ambalo watu wengine hawajaliona
Kujifunza kuna uwezo wa kukuamsha kwenye usingizi na kukufanya uwe macho
Kujifunza kutakufunulia yasiyoonekana na utakuwa na uwezo wa kuyaona
Kujifunza ndio moyo wa ugunduzi
Kujifunza kutakuondoa kwenye ufuasi na kukufanya kuwa kiongozi.

Yaani kujifunza kunaweza kukufanya uone ambayo hukuwahi kuyaona. Kunaweza kukufanya uende ambapo hujawahi kwenda. Kutakufanya pia ufike ambapo hujawahi kufika.

HIZO ZOTE NI FAIDA ZA KUJIFUNZA.
Hata hivyo mbali na faida zoote hizo za kujifunza watu hawachukui hatua kujifunza na hivyo kuendelea kubaki pale pale kila siku.

Usipojifunza unapata kutu. Mwisho wa siku utakatika kama chuma kilichopata kutu.
Robin Sharma jambo hili aliliweka vizuri aliposema “usipojifunza utakufa na umri wa miaka 20 na kusubiri kuzikwa ukiwa na miaka 80″.

Sasa rafiki kama kuna watu hawajifunzi basi hakikisha sio wewe. Yaani kamwe usiwe wewe.

Jifunze;
Kwa kusoma vitabu
Kwa kuangalia video zinazoelimisha
Kwa kuungana na watu waliofanikiwa kwenye sekta zao
Kwa mafanikio unayoyapata hata kama ni madogo
Kwa makosa unayofanya (madogo kwa makubwa)
Kwa makosa ya watu wengine.

Rafiki yangu, namalizia kwa kusema hivi. Jifunze tena na tena. Yaani kujifunza kufanye kuwe sehemu ya pili ya maisha yako.

Asante sana, tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X