Hatua Nne za Ukuaji Katika Uongozi


Kwa kawaida kila kitu huwa kina wakati wake. Kuna wakati wa kupanda wa kupanda na wakati wa kuvuna.

Katika maeneo yote ya maisha, yaani afya ya mwili, afya ya akili, afya ya roho, pesa, mahusiano na jamii pamoja na mahusiano na familia.
Huwezi kuwa kwenye kipindi kimoja kwa wakati mmoja.
Huwezi kuwa kuwa unapanda, unapalilia na kuvuna kwa wakati mmoja.

Hivyo lazima ufahamu hatua nne ambazo utazipitia wewe kama kiongozi wakati ukielekea kwenye mafanikio makubwa sana.

1. HATUA YA KWANZA NI HATUA YA KUPANGA
Hapa ndipo huwa tunapangilia kujua nini kifanyike na nini kisifanyike.
Katika hatua hii huwa tunaweka malengo, na hatua za kuchukua kuweza kufikia malengo haya.
Je, ni eneo gani la maisha yako upo kwenye kipindi hiki hapa.

Kama ni mkulima basi katika hatua hii ndipo unapaswa kuandaa shamba. Ili mvua zikinyesha uwe tayari kupanda

2. HATUA YA PILI NI KUPANDA
Ukishajua nini unapaswa kufanya na kuandaa mazingira ya kitu hicho,  basi kinachofuata ni kupanda. Katika hatua hii hapa ndipo unapaswa kupanda.
Hakikisha kipindi unakitumia vizuri la sivyo wakati wa mavuno wenzako watavuna na wewe utabaki tu kuwaangalia.

3. HATUA YA TATU NI  KUPALILIA
Haitoshi tu kwamba unapanda na unatulia. Bali unapaswa kufuatilia kile ulichopanda kuona kinaendeleaje. Je, kinahitaji nini ili kizidi kuzalisha zaidi na zaidi?

4. HATUA YA NNE NI KUVUNA
Kama hatua za mwanzo zote zilizopita ulizitumia vizuri, maana yake sasa hatua hii inakuhusua pia. Hapa ndipo sasa na wewe unaweza kushughulika na kuvuna kile ulichopanda.

Kumbuka usemi wa utavuna ulichopanda unafanya kazi ka iitwayo leo.

Rafiki yangu kitu kikubwa ni kwamba, hatua hizi hazirukwi. Unapaswa kufanya kile unachopaswa kufanya kwa wakati unaopaswa kukifanya ili uweze kupata kile unachohitaji kwa wakati unapokihitaji.

Huwezi ukawa unapanda kwenye kils kitu kwa wakati mmoja. Huwezi kuwa unavuna kwenye kila kitu kwa kwakati mmoja.
Kuna kitu utakuwa unapalilia, kingine unavuna, wakati kingine ndio bado unapanga au unapanda. Kwa siku zote jiulize, nipo kwenye hatua gani kwenye hiki nifanyacho?

Soma Zaidi:  Mambo Saba Ya Kujifunza Kutoka Kwa Simoni Petro

Asante sana rafiki. Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X