Hii Ndiyo Sehemu Unayoweza Kukimbilia Pale unaposhindwa Kutimiza Malengo Yako


Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Leo ni tarehe 10 ya mwezi wa 10, 2018. Zikiwa zimebaki siku 82 tu, mwaka huu kuisha.

Kama mwaka huu ulikuwa umeweka malengo makubwa sana sasa umefika wakati wa wewe kujiuliza ni wapi umeweza kufika katika suala zima la kutimiza malengo yako ya mwaka huu.

Jiulize umeweza kufanya nini? Uko wapi sasa na unaelekea wapi.

Rafiki yangu haya ni maswali muhimu sana ambayo unapaswa kujiuliza kabla mwaka huu haujaisha.

Sehemu ya kukimbilia @songambeleblog

Sasa rafiki yangu kama unavyojua hakuna kitu kinachopatikana kirahisi. Hakuna!! Na kama basi ulikuwa haujui, basi unapaswa kujua sasa hivi kwamba hakuna kinachopatikana kirahisi
Kadri unavyoweka juhudi, dunia nayo inaweka juhudi sana kuhakikisha inakurudisha nyuma. Kadri unavyojitahidi kufakinisha malengo yako, dunia nayo inakusukuma kukurudisha nyuma ili usiyatimize.

Ni katika hatua hii ambapo unahitaji kuwa king’ang’anizi wa hali ya juu sana.
Ni katika hatua hii ambapo unasikia hali ya kukimbia na kuacha kile ulichokuwa unafanya inaanza kukunyemelea.

Sasa unajua nini? Kama dunia ikikulazimisha kukimbia basi wewe kimbia kweli. Ila usikimbie kwa kuacha.
Badala yake kimbia kwa kuyaangalia malengo yako na ndoto zako.
Unaruhusiwa kukimbia ila usikimbilie sehemu nyingine tofauti na kukimbilia ndoto zako pamoja na malengo yako.

Je, ndoto zako umeziandika wapi? Je, unayo malengo?

Soma zaidi: Hatua Muhimu Katika Kuweka Malengo

KITABU, KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

Angalia ulipaswa kufanya nini katika malengo yako ambacho hujafanya? Ulipaswa kwenda wapi ambapo hujaenda?

Ni katika hatua hii ambapo utagundua uelekeo sahihi ambao unapaswa kukimbilia na hivyo kuifanya safari yako izidi kuwa rahisi na rahisi.
Ni katika wakati huu ambapo malengo yako yatakuonesha ni kitu gani sasa unapaswa kuboresha, na ni wapi ulikwama ili kusonga mbele.

Kama leo ninapaswa kukwambia kitu kimoja basi nitakwambia hivi,

Maisha yakikulazimisha kukimbia, kimbia kweli, ila usikimbie kwa kuacha malengo yako. Badala yake kimbia kwa kuelekea ndoto zako mpaka pale utakapokuwa umeweza kuzitimiza. Kimbia katika uelekeo wa kutimiza ndoto zako wala sio kuacha

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X