Hivi Ndivyo Unapaswa Kuishi Maisha Yako


Sasa hivi tunaishi katika ulimwengu ambao ni rahisi sana kupeleka kifaa kwenye mwezi kuliko ilivyo rahisi kumtmbelea rafiki yako.
Tupo kwenye ulimwengu ambao ni rahisi sana kuongea na watu wa mbali tukawasahau watu wetu wa karibu.
Tupo kwenye ulimwengu ambao ni rahisi sana ku kuchati na kuzurura kwenye mitandao ila kujikuta tunasahau kazi zetu.

Wakati haya yote yanatokea, siku zinazidi kusonga mbele.

Kuna namna ya kuishi ambayo tunapaswa kuiishi ila tunaisahau.
Na namna hii imewekwa vizuri kwa maneno haya machache yanayosema, ulipozaliwa ulilia wakati watu waliokuwepo wanacheka, unapaswa kuishi maisha kiasi kwamba utakapokufa ucheke wakati waliokuzunguka walie”

Je, haya ni maisha ya namna gani?
Maisha ya kuwasaidia watu
Maisha ya kutoa thamani kwa watu,
Maisha ya kubadili matatizo kuwa huduma au suluhisho,
Maisha ya kuwapenda watu wote.

Rafiki yangu haya ndio maisha unayopaswa kuyaishi kuanzia leo.
Kwa namna hii dunia itaweza kukumbuka vizuri sana!
Soma Zaidi: Mambo Saba (07) Ya Kujifunza Kutoka Simoni Petro

Asante sana rafiki yangu. Na hongera sana kwa zawadi ya siku hii ya leo.

Tukutane kwenye jukwaa lanwanamafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X