HIVI NDIVYO UNAWEZA KUENDELEA KUNG’AA KILA SIKU KATIKA SEKTA YAKO


Ni kawaida  ya binadamu kukua. Mtoto anapozaliwa huwa tunafurahia sana maendeleo yake. Kuanzia siku ya kwanza. Ile anapozaliwa tu, akilia kwetu huo tayari ni ukuaji na tunafurahia.
Baada ya hapo akianza kutambaa, kwetu hiyo ni faraja na furaha tena. 

Sio hilo tu, anapoanza kutembea, bado tunafurahi sana maana nyakati nzuri kama hizi hapa  zinakuwa zimejitokeza.

kwa hiyo ukuaji ni jambo endelevu ambalo tunapenda tuendelee kuliona likitokea maishani mwetu.
Ndio maana bado mtoto anapoingia shule ya msingi akahitimu, sherehe kubwa inafanyika. Kwa sababu ni hatua ya kipekee (ni ukuaji).
Vivyo anapoenda sekondari, chuo mpaka akiwa kazini (wakati anapanda vyeo)

Lakini sio watu wote huwa wanang’aa na kufanya makubwa kila siku. Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi ni watu wenye kazi kubwa sana. Hivyo kuna kipindi wanachoka sana na hivyo kupoteza morali ya kazi.

Lakini wewe hapo kuna kitu unapaswa kukifanya ili usipoteze motisha ya kazi kila iitwayo leo.
1. Hakikisha unafanya kile unachopenda
2. Hakikisha unakifanya unapopaswa kukifanya na kukiacha unapopaswa kukiacha.
3. Usivunje kanuni zako. Kama kuna kitu kitu umewahi kusema kwamba hutakuja kufanya. Usikifanye kwa ajili ya kumridhisha mtu ili na wewe uonekane umo!
4.. Fanya mazoezi  mara kwa mara. Yaani hakikisha kila siku unafanya mazoezi ya kile unachopenda kufanya.

5. Jenga timu bora kabisa iliyonyuma kukusaidia wewe kama kiongozi kufanya vizuri zaidi kila iitwayo leo.

Asante sana rafiki yangu. Na hongera sana kwa siku hii. Endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.

Mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa

Asante sana tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X