Huu Ndio Ukweli Ambao Watu Hawakuambii (Mlinganyo wa Maisha)


Hivi umewahi kuwa unaenda sehemu kumtembelea rafiki yako au ndugu ila bila kuwa na uhakika wa nyumba yake ilipo. Ukakaribia na sehemu ambayo ulikuwa unahisi kwamba hapa ndipo penyewe ila ukaja kushangaa kwamba mtu anayetokeza ni wa tofauti baada ya kugonga?

Ukaamua kuuliza kwamba kwa John ni hapa? ukaambiwa ni nyumbe ileee, huku ukioneshwa kwa kidole.
Je, ulijisikiaje?

Katika hali ya kawaida watu huwa tunapenda uhakika.
Na watu wengi wanapopata uhakika wanabweteka na kushindwa kuchukua hatua kubwa.

Kwa mfano leo hii wewe una uhakika na oksijeni, hivi ushawahi kujiuliza itakuwaje endapo nitaishiwa oksijeni? Kwa sababu ipo hata hujihangaishi nayo.

Jambo kama hili hapa ndilo huwafanya watu kutafuta mlinganyo sahihi wa maisha. Yaani huwafanya watafute kitu kilichonyooka maishani mwao. Ila ukweli ni kwamba hakuna mlinganyo ambao ni sahihi  kwa maisha.

Katika hesabu ni rahisi sana kujua kwamba saba mara saba ni 49.
Lakini katika maisha mlinganyo sahihi ni pale unapofuata kanuni, kuishi kadri ya malengo yako na kuamua kufuata kusudi la maisha yako.
Hapo unapaswa kufahamu kwamba hakutakuwepo na uharaka, wala hakuna njia ya moja kwa moja ya wewe kuweza kuyafikia mafanikio.
Njia rahisi ya kufikia mafanikio ni wewe kuchukua hatua kila siku na kuhakikisha unakuwa bora ya ulivyokuwa jana.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X