Moja kati ya kitu ambacho kimezoeleka sana miongoni mwa watu ni kupokea. Kila iitwayo leo, mtu anapenda kupewa na kupewa na kupewa.
Hivi kwa mfano sasa hivi ukikutana na mheshimiwa Raisi Magufuli, kitu gani kitakuja kwako kwanza?
Je, utafikiri kwamba akupe mtaji wa kuanza biashara?
Au utafikiri juu ya kukusaidia kupata ajira?
Je, utapenda akupe gari zuri la kutembelea?
Ni nini hicho kitakuja akilini mwako? Ni nini hicho?
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa sana ya watu kitu kitakachokuja akilini mwao ni kutaka kuona Mheshimiwa akitoa.
Wanataka waone anasema sasa ninaanza kujenga barabara. Sasa ninawaletea umeme, sasa ninawapa chakula n.k
Sheria za asili ni sheria nzuri sana. Sheria hizi zinakuhitaji wewe utoe ndipo upokee.
Na kadri unavyotoa ndivyo unavyopokea.
Jambo hili linaonekana ni geni machoni na gumu sana kumeza ila ndivyo ilivyo.
Kuna mfano wa bahari mbili zilizopo nchini Palestina.
Moja ya bahari hizi ina samaki, ina miti mizuri pembezoni, ina ndege wa kila aina wanaimba na kufurahi kwa shangwe, ina wadudu wa kila namna. Na katika bahari hii watu husafiri na hivyo kurahisisha ufanyaji wa biashara.
Katika bahari ya pili hakuna ndege, miti, samaki, watu hawasafiri kwenye bahari hii, na inaitwa bahari MFU!!
Je, nini kinatofautisha bahari hizi? Je, ni chanzo cha maji yake?
Hapana, maana ukiangalia mto unaoingiza maji kwenye bahari zote mbili ni mmoja, mto Jordan.
Tofauti yake ipo kwenye kutoa. Bahari moja ikipata tone la maji kutoka jordani inatoa tone jingine na hivyo kuifanya iwe bahari bora.
Bahari nyingine ikipokea tone la maji, inatunza kabisa bila kutoa hata tone la maji. Na hii ambayo haitoi maji ndiyo huitwa bahari mfu. Haina samaki, wanyama, miti mizuri ilizunguka, n.k
Kwa hiyo hapa tunaweza kuona kwamba kutoa ni jambo la maana sana kuliko kupokea.
Tujifunze kutoa zaidi na zaidi.
Na ukiangalia watu wanaoishi maisha mazuri dunia hii ni watu wanaotoa zaidi.
Mamilionea na mabilionea ni watu wanaotoa zaidi. Wanatoa huduma zaidi na kuwasaidia watu na hivyo wanapata zaidi ya wanavyotoa (ndivyo asili ilivyo)
Ukiangalia watu maarufu kama wanamziki ni watu ambao wanatoa zaidi ya wanavyopokea. Wanatoa kile kilicho ndani yao, kipaji na kuwanufaisha wengi zaidi.
Lakini kadri wanavyosaidia wengi zaidi ndivyo wanavyonufaika zaidi.
Rafiki yangu, na wewe unapaswa kujifunza kutoa. Sio lazima uanze kutoa kikubwa. Anza na hicho kidogo, tembea nacho mpaka utakapokuwa umeweza kufikia hatua kubwa sana.
Ni hayo tu rafiki yangu. Kwa siku ya leo. Yaani jifunze kutoa.
Je, unaenda kutoa nini?
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA