Rafiki yangu, hongera sana. Leo ni siku njema sana kuwahi kutokea kwenye dunia hii.
Ni siku ya kipekee sana kwetu kuchukua hatua kubwa sana.
Ni siku ya kipekee kuongeza mtandao wa watu wanaotufahamu.
Ni siku ya kipekee kwetu kutimiza malengo yetu.
Ni siku ya kipekee kwetu kuimarisha akili zetu na kujenga akili zetu kwa namna ya upekee sana.
Yaani ni siku ya kipekee katika kila kitu. Ikipita ndio imepita. Ukiifanikisha ndio umeifanikisha, na ukiipoteza ndio basi umeipoteza.
Sasa, leo naomba ufahamu kwamba ni siku unayopaswa kuwa na furaha zaidi ya siku nyingine yoyote kwenye maisha yako.
Leo unapaswa kuwa na furaha bila kujali nini kinatokea.
Huhitaji kusubiri mpaka machi 30 ambayo kidunia imewekwa kuwa siku ya furaha ili na wewe uwe na furaha.
Furaha yako inapaswa kuwa leo, tena sasa hivi.
Kwa kawaida furaha yako inapaswa kutokea ndani wala sio nje.
Au kiufupi ni kwamba unapaswa kufurahia wala sio kufurahishwa.
Anayefurahia anakuwa na furaha kutoka ndani yake.
Anayefurahishwa, furaha yake inatoka nje.
Je, wewe upo wapi.
Furaha ya nje ni ile ambayo inategemea mazingira.
Inategemea marafiki zako wasemeje juu yako. Inategemea pia mwonekano wako, kama nguo nywele na viatu.
Hivi ni vitu vya nje ambavyo huwa havidumu kwa muda mrefu. Maana yake ukivikosa ndio umekosa furaha yako.
Kwa mfano, kama furaha yako inategemea uvaaji. Siku ukikosa nguo nzuri zinazokufanya uwe na furaha ndio basi umepoteza furaha yako.
Au kama furaha yako inategemea watu wakusifie, siku ukikutana na watu wagumu kusifia ndio baasi, furaha yako imekwisha.
Rafiki yangu, kuwa na furaha siku zote, ila furaha yako isitegemee watu/vitu vya nje. Kamwe, usikubali mazingira yako yakutengeneze wewe.
Wewe ndiwe unapaswa kuyatengeneza mazingira.
Furaha yako inapaswa kutoka ndani. Kwa mfano furaha yako itokane na kutimiza kusudi lako la maisha. Au furaha yako itokane na kuwasaidia watu kufika hatua fulani.
Furaha yako itokane na jinsi unavyoishi. Uione kila dakika kama zawadi na hivyo nafasi ya kipekee ya kuwa na furaha.
Soma Zaidi; Watanzania Acheni Utani, Tamthiliya Hazijengi
Mimi Godius Rweyongeza furaha, wewe je?
Asante saana,
Nakutakia siku njema sana iliyojaa furaha tele, amani na busara zote.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA